Serikali yanunua vifaa tiba vya Saratani...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Salha Mohamed
SERIKALI imenunu vifaa tiba 100 vya tiba mgando ya mabadiliko
ya awali ya saratani ya shingo ya kizazi (cryotheraapy) huku Tanzania
ikiwa kinara wa ugonjwa huo Afrika.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kufungwa kwa mradi huo.
Hayo yamebainishwa leo wakati wa kufungwa kwa mradi wa
uchunguzi na matibabu ya awali ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi
uliofanyika miaka mitano kwa ushirikiano wa Chama cha Wazazi na Walezi (UMATI),
PSI na Marie Stopes kwa uwezeshwaji wa taasisi ya Bill and Gates.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mama
na Mtoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,
Dk Safina Yuna amesema mradi huo umesaidia kuboresha upatikanaji wa
mabadiliko ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi katika vituo 90.
"Kama mnavyojua Tanzania inaongoza kwa saratani ya
mlango wa kizazi hawa wametusaidia, Serikali imeamua kupanua wigo na
kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa."amesema.
Amesema takwimu zinaonesha wagonjwa wengi hufika hospitali ya
Ocean road wakiwa katika hatua za mwisho ambapo matokeo ya matibabu
yanakuwa si mazuri na kwamba mgonjwa akiwahi hupona.
Amesema vifaa tiba hivyo vitatumika kutibu matibabu ya awali
na upasuaji mdogo kwa wagonjwa wenye mabadiliko makubwa. Tayari vimeshasambazwa
katika vituo 466 nchini .
"Tutatanua zaidi kuhakikisha huduma zinawafikia walengwa
wengi ambao hawawezi kufika katika hospitali za wilaya na Mikoa pamoja na
vituo vya afya nchini."
Mkurugenzi wa Mifumo ya Afya ya Marie Stopes, Jeremia Makula
amesema mradi huo umefika katika mikoa 22 nchini.
"Katika kipindi cha maiaka 5 tumewafikia wanawake
187,267 katika uchunguzi wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi na
tumegundua asilimia 4.2 walikuwa na mabadiliko ya awali ya kansa ya
kizazi,"amesema.
Ameongeza kuwa wametibu wanawake 7600 sawa na asilimia 100 ya waliokuwa
wakihitaji matibabu ya awali ya mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango
wa shingo ya kizazi.
Amesema wanawake 1000 wamekuwa wakihitaji huduma ya juu
huduma ambapo walipewa rufaa ya matibabu katika hospitali zinazotoa huduma
hiyo.
Makula amesema katika mradi huo wameanza kutumia kipimo kipya
ambacho hakijawahi kutumika hapa nchini licha ya kuwa na changamoto nyingi
katika kuwafikia waliokuwa vijijini.



No comments:
Post a Comment