Polisi Dar wamshikilia Sheikh Issa Ponda..Soma habari kamili na Matukio360..#share
JESHI la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Sheikh Issa Ponda kwa tuhuma za
uchochezi.
Sheikh Issa Ponda
Kukamatwa huko ni baada
ya Sheikh Ponda akiwa na mawakili wake leo kujisalimisha katika kituo cha kikuu cha
kati cha Polisi kutii agizo lililotolewa hivi karibuni na mkuu wa polisi kanda
maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.
Wakili wa Sheikh
Ponda, Profesa Abdallah Safari ameiambia Matukio360 kuwa hadi sasa Polisi
wanamshilia Sheikh Ponda na kwamba dhamana
ipo wazi.
Polisi wametaka watu
watatu wa kumuwekea dhamana Sheikh Ponda, mmoja wapo lazima awe mtumishi wa
serikali.
Hivyo hadi muda huu
tumeshapata wadhamini wawili bado mmoja hivyo muda wowote ataachiwa kwa
dhamana.
Profesa Safari ambaye
pia ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA amesema Sheikh Ponda anashikiliwa kwa
tuhuma za uchochezi.
pamoja na mambo
mengine Ponda anashikiliwa
Hivi karibuni Sheikh
Ponda alitoa taarifa mbalimbali kutokana na matukio yanayoendelea ikiwamo
mwenendo mzima wa mauaji, maiti kuokotwa, raia na viongozi kadhaa kutekwa na
kupotea
Katika mkutano wake na waandishi wa habari Sheikh Ponda alisema Watanzania wamekata tamaa
na usalama wao na wanaishi kwa hofu na
kwamba kama Serikali inawajibika ipasavyo matukio hayo yasingekuwepo.
‘’Serikali imekuwa
ikiwaandama baadhi ya viongozi wa dini na wa vyama vya siasa hasa vya upinzani,
wakati viongozi hao ndiyo wanaoikumbusha
serikali wajibu wake na sasa wamekuwa
wakifikwa na hatari ikiwamo kupata vilema vya kudumu.’’ Na kuongeza ‘’Mimi
binafsi nilipigwa risasi hadharani mwaka 2013
na hivi sasa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Tundu Lissu
.’’
Sheikh Ponda aliiomba
Serikali kuacha kuwazuia viongozi wa upinzani kuzungumza mambo mbalimbali
yahusuyo nchi.
‘’Serikali imezuia
haki za kidemokrasia kwa viongozi wa upinzani. Imezuia kufanya mikutano ya
hadhara na maandamano ya amani.’’



No comments:
Post a Comment