TRA Yakusanya Sh.Trilioni 3.65..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

Na Hussein Ndubikile

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu imekusanya jumla ya Sh Trilioni 3.65.
Image result for kayombo tra
Aidha, imesema  makusanyo hayo ni  sawa na asilimia na ukuaji wa asilimia 1.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha wa 2016/17.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaama na Mkurugenzi  wa Huduma na Elmu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya kipindi cha robo  ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18.

Amesema katika kipindi cha mwezi Julai Sh trilioni 1.101 trilioni, Agosti Sh trilioni 1.205 huku akibainisha kwa mwezi Septemba mwaka huu jumla ya Sh trlioni 1.345.

“Kwa makusanyo haya, TRA inapenda kuwashukuru wafanyabiashara kwa wananchi wote kwa ujumla kwa kuendelea kulipa kodi na kuiwezesha Serikali kutimiza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi,” amesema Kayombo.

Aidha, amesema mamlaka hiyo ianwakumbusha wafanyabishara wote kutoa risiti za kielektroniki kwa kila mauzo na kudai risiti kwa kila manunuzi kwani ni njia pekee ya kupata mauzo sahihi yanayoiwezesha TRA kukokotoa kodi sahihi na kwa haki.

Amewakumbusha wananchi wote kuhakiki risiti zao ili kuona usahihi wa taraehe na kiasi walicholipa na bidhaa waliyonunua kabla ya kuondoka na risiti hizo.

Amewasisitiza wananchi kutoa taarifa kwenye ofisi za TRA walizokaribu nazo au vituo vya huduma kwa wateja endapo wataona risiti hazina vigezo.

Aidha, amewakumbusha wamiliki wa majengo nchini kulipa kodei ya majengo mapema badala ya kusubiri mwishoni mwa mwaka wa fedha ili kuepuka msongamano na usumbufu usio wa lazima.

Pia , ametoa wito kwa wafanyabishara wa michezo ya kubahatisha kulipakodi zao kwa mujibu wa sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41.

Pia , ametoa wito kwa wafanyabishara wa michezo ya kubahatisha kulipakodi zao kwa mujibu wa sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search