TAARIFA KWA UMMA KUHUSU FISI ALIYEUAWA KITUO CHA MABASI CHA UBUNGO-DAR ES SALAAM..

Tarehe 23/09/2017 ilitolewa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mnyamapori  (fisi) aliua katika kituo cha mabasi ubungo, Dar es Salaam. Taarifa hiyo iliambatana na picha ya video video clip inayoonyesha watu waliovaa mipira ya mikononi Gloves na wengine wengi wakiangalia fisi mmoja aliyekuwa amelala chini akionekana amekufa. Taarifa zilisema askari wa usalama barabarani wa kituo hicho cha mabasi walimpiga risasi mnyama huyo.
Kufuatia taarifa hiyo, Mamlaka ya Usimamizi wanyamapori Tanzania (TAWA) tulifuatilia na kubaini kuwa hakuna fisi wala mnyamapori yeyote anayefanana naye aliyeuwa kituoni hapo tukathibitisha kuwa ni uzushi na uongo. Hatua tulizopitia kuthibitisha haya ni kama ifuatavyo:-
Hakuna taarifa ya tukio katika vituo vya polisi na  Ofisi ya Manispaa ya Jiji inayosimamia uendeshaji wa huduma katika kituo hicho
Hakuna majengo katika kituo hicho wala jirani yanayofanana na yale yanayoonekana katika clip hiyo
Kutokana na mahusiano mazuri kati ya TAWA na vyombo vingine vya usalama, tungeitwa kushiriki kumthibiti mnyama huyo kama angetokea kuwepo
Tunaomba Umma upuuze taarifa hiyo kwani siyo ya kweli.

Limetolewa
Na
KAIMU MKURUGENZI MKUU-TAWA

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search