Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Dar lazindua mpango wa huduma za dharura,,,Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Hussein Ndubikile
JESHI la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Dar es Salaam limezindua Mpango wa kukabiliana na huduma za dharura.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Hashimu Mgandilwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango wa huduma ya dharura kwa jeshi la zimamoto na uokoaji akiwa pamoja na wageni wengine.
Akizindua mpango leo huo Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashimu Mgandilwa amesema mpango umetekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Maafa ya mwaka 2015 na kwamba utasaidia kupunguza uwezekano wa kutokea majanga jijini humo.
“Mpango huu umerudisha mfumo wa awali wa maisha lengo ni kukabailiana na dharura za jijini Dar es Salaam tunaimani utaokoa maisha ya wananchi hasa pale yanapotokea majanga mbalimbali,” amesema.
Amebainisha kuwa mpango huo umefadhiliwa wadau wengi wakiwemo Benki ya Dunia(WB) ambao ndio wafadhili wakuu pamoja na Shirika la Misaada na Maendeleo la DFID.
Ameipongeza Serikali ya mkoa huo kwa kutekeleza sheria hiyo huku akiwasihi watakaopatiwa vifaa vya dharura kuvitumia kwa uangalifu ili visiharibike.
Pia, ameziomba halmashauri kuweka utaratibu wa kutenga fedha zitakazokuwa zikitumika wakati maafa yanapotokea.
Kwa upande wake Mratibu wa Mpango huo, Dkt. Christopher Mnzaki amesema mpango wa huduma hiyo umeanza katika wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke huku akisisitiza umekubaliwa na Tamisemi na tayari mafunzo yashatolewa.
Amesema mpango huo hautaishia katika wilaya tatu bali utasambaa katika wilaya nyingine lengo likiwa kupunguza madhara yanayoweza kutokea kutokana na majanga yakiwemo ya mafurikio na moto.
Amefafanua kuwa bado wanakabiliwa na uhaba wa magari ambapo hivi sasa kuna magari 46 yanayofanya kazi 12 ila magari sita pekee ndio yenye uwezo wa kufanya kazi ipasavyo.
Naye Mkurugenzi wa Menejimenti ya Majanga- Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amekabidhi eneo kwa jeshi hilo litakalotumika kuhifadhi vifaa vya dharura na kuipongeza Serikali ya mkoa huo kwa kuonyesha mfano wa kuigwa.
Mratibu wa mpango wa huduma ya dharura kutoka (DarMaert) Dk.Christopher Mnzaki akizungumza pamoja na kutoa maelezo juu ya mpango huduma hiyo iliyozinduliwa siku ya leo
No comments:
Post a Comment