TCRA wateta na viongozi wa Dini...Soma habari kamili na Matukio360..#share

Na Abraham Ntambara




VIONGOZI wa Dini nchini wametakiwa kuongeza jitihada za mafunzo ya kiroho na maadili kwa waumini ili kutojiingiza katika makosa ya kimtandao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhad Mussa Salum.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Kimtandao, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Joshua Mwangasa  katika semina ya matumizi bora ya simu na mitandao ya kijamii kwa vingozi wa dini Mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Amesema sababu kubwa ya jamii kuingia katika uhalifu wa makosa ya kimtandao ni ukosefu wa maadili, kutoelewa vizuri sheria ya mtandao na baadhi ya watu kutoheshimu utu wa mtu.

"Chanzo kikubwa ni ukosefu wa maadili, hivyo watu hawathamini utu wa mtu mwingine , tunawaomba viongozi wadini ujumbe huu ufike kwa waumini, muwafundishe maadili," amesema Mwangaza.
 Mkuu wa Kitengo cha makosa ya kimtandao wa Jeshi la Polisi




Mkurugezi wa TCRA James Kilaba  amewataka viongozi hao kutumia elimu waliyoipata na kuwaelimisha waumini kutokubali  kupokea na kusambaza tarifa zisizofaa na badala yake walipoti vituo vya polisi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhad Mussa Salum amesema elimu waliyoipata itakuwa ni wimbo  wa kueleimsha jamii kuhusu matumizi sahihi mitandao kwa kufuata sheria za .


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search