TECNO kuja na Smartphone yenye ‘internal memory’ kubwa..Soma habari kamili na Matukio360..#share
ZILE zama ambazo ule ujumbe wa "hauna
nafasi ya kuhifadhi vitu kwenye simu yako" ulikua unaboa sana kwenye
smartphones zetu, zishapitwa na wakati. Hakika tumeona Tecno wakijaribu
kutusaidia katika tatizo hilo kwa kutuletea simu ambazo zina uwezo mkubwa sana
wa kuhifadhi vitu, yaani internal memory. Tuchukulie mfano simu ya Phantom 6
plus ambayo ina ukubwa wa 64GB kama internal memory. Hongereni sana Tecno
katika hilo.
Tukizungumzia memory, tunaongelea vitu
viwili, ROM na RAM. Kiufupi ROM ni ule ukubwa wa nafasi ya kuhifadhi vitu
katika simu yako na RAM ni kitu inayowezesha simu yako ifanye kazi kwa uharaka
bila ya kustack.
Tecno wamefanya kazi nzuri sana katika vitu
hivyo viwili. Sasa basi kwakua Phantom nyingine ipo njiani inakuja, ni dhahiri
kua tunategemea vitu vizuri na vikali zaidi. Phantom 6 plus ilikua kiboko, huku
nina kitu cha 64GB ya ROM, kule nina 4GB za RAM, yaan ulikua ni mwendo wa
kucheza magemu tu makubwamakubwa kwa kasi ya ajabu.
Hakika sitarajii kitu chochote pungufu katika
huyo bwana mkubwa Phantom anayekuja. Nitafurahi sana kama Phantom inayokuja
itakua na uwezo wa ROM sio chini ya 64GB, au hata kama wakiamua kunibariki na
kitu cha 128GB itakua fresh. Tukija kwenye RAM palee..tafadhali tuleteeni 6GB
hizo. Ebhana kama Phantom inayokuja itakua imebeba hiyo mizigo, lazma niitie
mkononi.
Sasa kwa wale wote wachezaji magemu sana,
hakika RAM itawatendea vyema sana. Na kwa wale wenzangu wa kuangalia mamuvy
nini kwenye simu, internal storage kubwa hiyo itakuwezesha uhifadhi mamuvy
kibao tu.
Basi wote tukae mkao wa kula… Kitu cha
Phantom kinakuja.






No comments:
Post a Comment