Serikali kununua ‘vichwa’ vya Magufuli..soma habari kamili na Matukio360..#share

 SERIKALI ya Tanzania inatarajia kununua vichwa 15 vya treni ambavyo Rais Magufuli alivikuta bandarini vikiwa havina mwenyewe mwanzoni mwa mwezi Julai, 2017. Pia imeunda tume ya watu 11 kuvichunguza.
Vichwa vya treni vilivyopo Bandarini

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema kuwa serikali imekusudia kuvinunua vichwa hivyo vya treni kwa matumizi endapo vitakuwa ni vizima na kama havitakuwa na matatizo yoyote.

Prof. Mbarawa amesema endapo vichwa hivyo vikionekana ni vizima kwa mujibu wa uchunguzi ukaofanywa na tume hiyo ya watu 11 iliyoundwa na serikali hivyo serikali itakaa chini na mmiliki wa vichwa hivyo 15 vya treni na kuzungumza naye biashara. 


Mwezi Julai Rais Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam alisema ameviona vichwa vya treni zaidi ya 15 ambavyo kwa muda huo vilikuwa vinaonekana havina mmiliki, na kudai kuwa vichwa hivyo vya treni ni vibovu. Rais aliagiza Wizara husika kulifanyia kazi jambo hilo ili ukweli ufahamike kuhusu vichwa hivyo 15 vya treni.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search