TMA yatabiri mvua kubwa.. yawataka wananchi kujihadhari.. soma taarifa kamili na matukio360.. #share

Na Salha Mohamed

MAMLAKA ya hali ya hewa nchini(TMA), imewatahadharisha wananchi kunyesha kwa mvua kubwa ndani ya saa 24.


Mvua hiyo iliyozidi milimita 50 inatarajiwa kunyesha kuanzia Oktoba 31 hadi Novemba 3, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo, imesema kuwa kiwango cha mvua hiyo ni cha uhakika wa juu kwa asilimia 80.

Taarifa hiyo imeainisha baadhi ya maeneo yatakayoathirika zaidi kuwa  Tanga, Dar es Salaam Pwani pamoja Visiwa vya Unguja na pemba.

Pia kuelekea Novemba 3 mwaka huu,  mvua hiyo inatarajia kusambaa katika maeneo ya Mkoa wa Lindi

Hali hiyo ni kutokana na kuwepo na kuimarika kwa ukanda wa mvua (Inter  tropical Convergency Zone-ITCZ)  katika maeneo hayo.

Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo yaliyotajwa na kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zilizotolewa huku ikiendelea kutoa mrejeo kila itakapobidi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search