UPDATES: ZITTO KABWE AACHIWA KWA DHAMANA BAADA YA 'MSOTO' POLISI KWA SAA 10.. Soma taarifa kamili na matukio360.. #share
Ni takriban Saa 10.5 Jioni
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Polisi tangu saa 12 asubuhi.
Akithibisha kuachiwa kwake, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema, Zitto amehojiwa kwenye vituo viwili tofauti. Kwanza alihojiwa kwenye Kituo cha polisi Chang'ombe kwa kile kilichosemwa kutoa kauli za uchochezi Wakati wa ufunguzi wa kampeni za udiwani kata ya Kijichi. Aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti polisi siku ya Jumatatu ya wiki ijayo.
Kabla hajaondoka kituo cha Polisi, Zitto alikamatwa tena na kupelekwa Ofisi ya DCI iliyopo Mtaa wa Kamata, Kariakoo. Hapa alihojiwa kuhusu Tamko la Kamati Kuu ya ACT Wazalendo Kuhusu Kusinyaa kwa Uchumi. Baada ya mahojiano ameachiwa tena kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena siku ya Jumanne ya wiki ijayo.

No comments:
Post a Comment