Tundu Lissu ampa ujumbe maalum Sheikh Ponda..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
SHEIKH Issa Ponda amesema Rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ameahidi kuendelea na harakati za ukombozi na
kupigwa kwake risasi kumemuongezea ujasiri zaidi.
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
Ponda ameyasema hayo leo katika mkutano wake na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kwamba afya ya Lissu inaendelea
kuimarika.
‘’Hivi karibuni nilikuwa nchini Kenya alikolazwa Lissu
kumjulia hali yake, kumuombea dua na kumjengea matumaini ya afya yake na
matumaini endelevu ya harakati zake za umma na kujenga mazingira ya kutosha ili
niweze kuzungumzia ipasavyo matukio ya
mauaji, kuokotwa kwa maiti na kubanwa kwa uhuru wa viongozi na raia kuzungumza
na kukemea maovu .’’
Amesema walizungumza vya kutosha na kwamba Lissu ameahidi
pindi atakaporejea nchini ataendeleza mapambano na kamwe hawezi kukaa kimya.
‘’Amenieleza kazi muhimu anazofanya akiwa pale
kitandani huku akiamini damu yake na yangu na zingine zitakazomwagika kwa namna
hii zitawalipa watanzania kwa kupata uhuru wa kweli wenye thamani.’’ amesema
Sheikh Ponda amesema amehimizwa na Lissu mshikamano
huku akiwa na matumaini ya kuwepo watu kama yeye wenye fikra na matumaini ya
kuifikisha nchi sehemu salama.
Amesisitiza na kuwataka Watanzania kuwa na nguvu ya pamoja katika kutetea maslahi
ya taifa.
‘’Wanaoamini
hali iliyopo sasa inatokana na serikali kushindwa kutekeleza wajibu wake
tuunganishe nguvu kuhakikisha serikali inatekeleza wajibu wake.’’
Sheikh Ponda amewataka viongozi wa dini, wasomi,
viongozi wa vyama vya upinzani na viongozi
wa CCM waiambie Serikali ukweli.
No comments:
Post a Comment