#Updates Kutoka Kituo cha Polisi Kamata.. Zitto abanwa kwa makosa manne(4).. soma habari kamili na matukio360.. #share
Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa Polisi wanaendelea na mahojiano na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe baada ya kumuachia Kituo cha Chang'ombe kwa dhamana na kumtaka arudi siku ya Jumatatu, na kisha kumkamata tena na kumleta kwa mahojiano katika kituo cha Polisi cha Kamata.
Mahojiano ya sasa yanahusisha tuhuma mbili:
1. Kuchapisha takwimu kinyume na Kifungu cha 37(5) ya Sheria ya Takwimu 2015, Polisi wakitafsiri kuwa kusoma kwake taarifa ya Kamati Kuu ya ACT Wazalendo iliyofanya kwa kina uchambuzi wa takwimu za Serikali juu ya hali ya uchumi wa nchi kusinyaa, kuwa ni kuchapisha Takwimu.
2. Kusambaza taarifa hiyo ya Uchambuzi ya Takwimu ya Kamati Kuu ya ACT Wazalendo kwenye mitandao ya Kijamii kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Mitandao ya Kijamii (Cyber Crime Act).
Akiongea na matukio360 mchana huu, Ado Shaibu, Katibu - Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma amethibisha kuwa mpaka sasa jumla ya tuhuma ni nne, kwa kuunganisha zile mbili za awali za Uchochezi kwa kuwakataza wananchi wasiichague CCM kwa sababu mpaka leo Serikali ya CCM imeshindwa kuwakamata waliompiga risasi Lissu pamoja na kushindwa kujua chanzo cha maiti mbalimbali zinazookotwa katika ufukwe wa Coco Beach.

No comments:
Post a Comment