UZINDUZI WA DUKA KUBWA KABISA LA SIMU NCHINI TECNO SMART HUB MLIMANI..#share
KAMPUNI ya simu nchini TECNO imezindua duka kubwa zaidi la simu za
mkononi “TECNO SMART HUB” lenye ukubwa wa mita za mraba 110, duka hilo lenye
uwezo wa kuhudumia takribani wateja zaidi ya 50 kwa mara moja.
(Menea Daniel Xu akizindua na kuwakaribisha wadau wa TECNO)
Wakati wa uzinduzi huo, meneja wa kampuni ya simu za TECNO Bw. Daniel xu, aliongoza wateja waliofika kushuhudia uzinduzi wa SMART HUB HIYO kukagua na kujionea uzir wa duka duka hilo jipya huku akitoa maelezo kwa wageni walioalikwa kazi mbalimbali za vitengo vilivyomo katika duka hilo, TECNO imezindua duka hili maalumu ili kuwapa wateja wake huduma bora na za kisasa Zaidi kuwahi kutokea katika ulimwengu wa biashara za simu za mkononi nchini.
Aidha wateja
pamoja na wageni waalikwa wali furahia kuhudhulia uzinduzi huo baada ya kupata
elimu ya jinsi ya kutunza simu za kisasa “smart phones” vizuri hasa kwa
watumiaji wapya wa simu hizo. Lakini kwa sasa TECNO wameweza kuweka mafundi wao
kwenye TECNO SMART HUB hiyo kubwa, ambapo pia wanatoa huduma za ushauri pamoja
na kutengeneza simu kwa ustadi wa juu kabisa
endapo simu ya mteja itakua na
tatizo lolote.
Uzinduzi wa TECNO
SMART HUB, uliendana sambasamba na burudani za aina mbalimbali ikiwemo muziki
na vinywaji vilivyotolewa bure kwa wateja wa TECNO waliofika katika eneo la
tukio.
Kampuni ya simu za TECNO, ndio kampuni inayo
ongoza kwa kutoa simu za kisasa zenye ubora wa hali ya juu pamoja na huduma
bora zaidi, kuliko kampuni yoyote nchini. Na kupitia duka lao hilo utafurahia ulimwengu
wa simu bora za kisasa uliojaa huduma bora za kujali wateja.
(Muonekano wa
duka jipya la TECNO SMART HUB lililopo Mlimani City)
(Eneo la
mapumziko na vipuli/accessories za simu)
(Mteja akipata maelekezo na
ufumbuzi kutoka kwa mtoa huduma wa TECNO)
(Sehemu ya
duka, eneo la display za simu)
Sehemeu ya wateja kupumzika wakusubiri
huduma
No comments:
Post a Comment