Waziri Mkuchika Aanza Kazi kwa Kuwapiga Mkwara Mzito Watumishi wa Umma..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika, ameweka wazi mipango yake katika kutumikia nafasi yake na kusema yeye ataanza kuhakikisha watumishi wa Umma wanatumia muda wao kufanya kazi na hataki kusikia watumishi wameondoka kazini kwa ajili ya kwenda kunywa chai.

Mkuchika ametoa kauli hiyo leo Oktoba 10, 2017 baada ya  kuapishwa na Rais John Magufuli kuwa Waziri katika wizara hiyo, amesema kuwa katika kipindi chake atahakikisha wafanyakazi wanalipwa mshahara kulingana na kazi zao kweli, na wanatumia muda wa kazi kufanya kazi za serikali.

"Kwanza katika kipindi changu nikiwa Waziri kwa watumishi wa Umma, nataka wananchi wanapofika maofisini wawakute maofisini, mara nyingi wengi wanaripoto ofisini baada ya muda wanaondoka wanasema wanaenda kunywa chai, yaani wananchi wanatoka vijijini wanamsuburi mtumishi aje eti ameenda kunywa chai jambo hili kuanzia leo nitasimamia kuhakikisha watumishi wa umma wanashinda kazini kwao ili kila mtumishi wa Umma alipwe mshahara kwa kufanya kazi muda wote" alisema Mkuchika

Aidha Mkuchika amesema kuwa kwa sasa watumishi wengi wa Umma wanalipwa mshahara kamili kwa kufanya kazi robo za serikali jambo ambalo yeye atakwenda kulisimamia na kuhakikisha kuwa watumishi hao wanafanya kazi kamili ili walipwe kulingana na kazi zao kamili.

Mbali na hilo Mkuchika amedai kuwa atakwenda kuongea na Waziri wa Elimu ili ikiwezekana somo la Rushwa lianze kufundishwa kuanzia shule ya awali nchini mpaka vyuo vikuu na kusema watu wamekuwa wakichukua na kutoa rushwa kwa kuwa hawana elimu ya kutosha juu ya athari ya rushwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search