Wananchi waliovamia reli watakiwa kuondoka kwa hiari...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imewataka wananchi
waliovamia na kujenga makazi katika
maeneo ya miundombinu ya Reli kubomoa nyumba zao kwa hiari yao kabla serikali haijawasaidia kufanya hivyo.
Naibu Waziri wa ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye, akieleza jambo mbele ya baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri
wa Wizara hiyo Atashasta Nditiye alipotembelea Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na
kuelezwa kuwa imeanza kuboresha miundombinu kwa ajili ya kurejesha safari za
treni kutoka Tanga kuelekea Kilimanjaro
hadi Arusha.
“Kwa hiyo wale ambao wamevamia maeneo ya reli wabomoe
wengine, vinginevyo tutawasaidia na hata fidia ikibini ya kuwabomolea
tutawadai,” amesema.
Aidha amesema kwa wale ambao walikuwa wamejenga kwa vibali
harali na kufuatwa na miundombinu ya reli watalipwa fidia lakini kwa waliovamia
hawatalipwa.
Amewataka wananchi katika maeneo yote nchini ambayo reli inapita kuhakikisha wanapisha ili ujenzi wa reli kwa kiwango cha Standard Gauge ufanyike bila vikwazo na kukamilika mapema.
Kwa upende mwingine amewataka watumishi wa TRL kufanya kazi
kwa kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kuhakikisha wananchi
wanahudumiwa vizuri kwa usafiri wa njia ya reli kwani atakayekwenda kinyume serikali
haitamvumilia itamchukulia hatua za kisheria.
Akizungumzia kuhusu kuboreshwa kwa reli ya kutoka Tanga
kuelekea Kilimanjao hadi Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Masanja Kadogosa,
amesema maboresho hayo wameanzia Korogwa na sasa wamesakarabati kilometa
20 hadi Mombo na lengo ni kuanzia
mwakani treni zianze safari kupitia reli hiyo.
Aidha amesema kinachowasukuma kufanya maboresho hayo ni kwa ajili
ya kusaidia maendeleo ya kiuchumi pamoja na kusafirisha abiria na mizigo
nchini.
Akizungumzia ujenzi wa Reli ya Standard Gauge amesema hadi
sasa maendeleo ya ujenzi huo ni mazuri na kwamba wamekwisha fanya usanifu na
wemeanza ujenzi wa matuta pamoja na kambi.
Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni wa TRL Focua Sahani
amemweleza Naibu waziri kuwa Kampuni hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu
wa wafanyakazi, wanahitaji vichwa visivyopungua 45 na kuboresha mabehewa 17.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Masanja Kadogosa akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri Atashasta Nditiye.
No comments:
Post a Comment