Waziri Mwijage mgeni rasmi tamasha la maonesho ya magari..Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Salha Mohamed
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la maonesho ya magari
litakalofanyika Oktoba 27 hadi 29, 2017 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Vision Investiment, Ally Nchahaga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu maonesho ya 10 ya tamasha la magari litakalozinduliwa na Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage Oktoba 27,The Green jijini Dar
es Salaam.
Maonesho hayo ya siku tatu yameandaliwa na Kampuni ya New
Vision yatafanyika katika viwanja vya The Green, lengo likiwa kuonesha
bidhaa za vyombo vya moto na huduma kwenye vyombo vya moto,kupata elimu
na kuridhishwa navyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam,
Mratibu wa Maonesho hayo, Ally Nchahaga amesema maonesho hayo yatafungwa
Oktoba 29 na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi.
"Tuko hili linahusisha moja ya maonesho muhimu sana na
enye mvuto katika ulimwengu wa vyombo vya moto,matoleo mapya ya pikipiki na
burudani kwa ajili ya familia,"amesema.
Amesema watu wengi wanashindwa utunzaji sahihi wa magari
kutokana na kukosa elimu kwan magari ya sasa mengi hutuma teknolojia na si
kama ya zamani.
Nchahaga amesema tamasha hilo ni muhmu katka vyombo vya moto
kwa kuonesha magari ya abiria, biashara, pikipiki, bodi za magari, sehemu za
magari, mashine, huduma shirikishi na zana zinazohusika na magari.
Amesema katika maonesho hayo kutakuwa na burudani ambapo
wapenzi wa magari wataonesha ujuzi wa kucheza na vyombo vya moto
ambayo itawaburudisha watoto na kuwaelimisha usalama barabarani.
Kwa upande wake mdhamini wa Tamasha hilo ambaye pia ni Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Bima ya Britam, Oscar Ruhasha amesema watatoa
elimu ya bima kwa vyombo vya moto kwani watu wengi hawana elimu hiyo.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya kuuza magari ya Hyundai, Anthony
Nyeupe amesema kupitia tamasha hilo wananchi watapata fursa ya
kubadilishana mawazo na kuonesha bidhaa zao mpya.
No comments:
Post a Comment