Wataalam wa Udhibiti Ubora wa Dawa Afrika Mashariki Wakutana Jijini Dar..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
KATIKA kukabiliana na bidhaa zisizo na ubora katika jumuiya ya Afrika mashariki wadau wa Jumuiya hiyo
wamekutana katika mkutano utakaojadili
uainishaji wa kanuni za ushughulikiaji wa dawa pamoja na vifaa tiba kwa nchi za Afrika mashariki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza alipokuwa akifungua kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo leo jijini
Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya amesema
mkutano huo una lengo la kuweka
utaratibu kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na utaratibu wa kuleta
bidhaa za afya kutoka nje nchi zenye viwango vya ubora unao fanana.
Aidha amesema lengo la Jumuiya ni kwamba ifikapo
mwishoni mwa mwaka huu bidhaa yoyote inayoingia katika nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki ziwe na ubora huo.
"Mkutano huu ni muedelezo wa hatua ambazo zilianzishwa 2012 ili kuhakikisha nchi zote katika ukanda huu za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinakuwa na tarati zinazofanana kwa kuleta bidhaa za afya kutoka nje ya nchi zinazokuwa na viwango vya ubora vinavyofanana," amesema Dk. Ulisubisya.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Hiiti Sillo amesema
kupitia kikao hicho cha Kamati Tendaji Kinachosimamia utekelezaji wa mfumo wa pamoja
wa jumuiya ya nchi za Afrika mashariki unaosimamia masuala ya udhibiti na ubora
wa usalama wa dawa na bidhaa nyingine, amebainisha kuwa kamati hiyo inapokea taarifa za
kamati tendaji za wizara za afya ambayo ni pamoja na kuwa na miongozo inayofanana ya Jumuiya hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayepia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Udhibiti Dawa Afrika Mashariki Hiiti Sillo akielezea jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wataalam toka taasisi hizo leo jijini Dar es Salaam.
Aidha Sillo amesema mifumo ya udhibiti nchini
Tanzania ni mifumo inayoongoza huku
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Msajili wa Dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Dk. Shani Maboko akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.Picha na: Frank Shija – MAELEZO
No comments:
Post a Comment