Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Awataka Wanafunzi Wakike Wasishawishike..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule mbalimbali nchini kusoma kwa bidii na wasikubali kushawishika.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimia na wanafunzi Kike wanaosoma WAMA_SHARIF Sekondari .iliyopo Mkoani Lindi .Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kkikwete (MB) Waziri Mkuu ametembelea shule hiyo jana Oktoba 4,2017 alipokuwa katika ziara ya siku moja katika Mkoa wa Lindi jana.
Pia Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka sheria kali kwa wote watakaobainika kukatisha masomo ya watoto wa kike kwa kuwapa ujauzito au kuwaozesha.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Oktoba 04, 2017) wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana na WAMA Sharaf.
Shule ambayo ipo wilayani Lindi inamilikiwa na Taasisi ya WAMA ambapo inasomesha watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira magumu.Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao wa kike kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa bidii na hatimaye watimize malengo yao.
Amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia vizuri fursa hiyo ya elimu wanayoipata shuleni hapo kwa kusoma kwa bidii na wafuate ratiba itakayokuwa inapangwa.“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikubali kushawishika na kukatisha masomo yenu.”
Naye, Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Kuteuliwa alisema shule hiyo inasomesha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kutoka mikoa yote nchini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ahamasisha utunzaji wa mazingira Nchini kwakupanda Mti jana Oktoba 4/2017 katika Shule ya WAMA_ SHARIF SEKONDARI.iliyopo Mkoani Lindi ,kushoto mwenye fimbo ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Daktari Hamisi Kigwangala na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (MB) Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku moja jana Mkoani Lindi .PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, OKTOBA 05, 2017.
No comments:
Post a Comment