Naibu Waziri atembelea TAWA... soma habari kamili na Matukio360... #share
Dkt. Felician Kilahama (Mwenyekiti wa Bodi TAFORI) Naibu Waziri Maliasili na Utalii Japhet Ngailonga Hasunge mbele ya watumishi wa TAWA na TAFORI
Mhe. Naibu Waziri kabla
ya kuongea na watumishi wa TAWA alifika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa
ajili ya kujitambulisha kwake na kupokea taarifa fupi kutoka kwa Dkt.Stephene
Kebwe( Mkuu wa Mkoa wa Morogoro). Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Dkt.James
Wakibara (Kaimu Mkurugenzi Mkuu-TAWA), Edgar Masunga (Kaimu Mtendaji Mkuu
–TTSA), Kaisi Mwaikambo (Kaimu Mkurugenzi Mkuu-TAFORI) na Bw.David Kanyatta
(Kaimu Mkurugezi Huduma za Raslimari wanyamapori –TAWA). Mkuu wa Mkoa alimueleza Naibu Waziri kwamba Mkoa wa Morogoro umebalikiwa kuwa na
Hifadhi nyingi za Wanyamapori ikiwemo Pori la akiba kuliko yote barani Afrika,
Pori la Selous.
Mkuu wa Mkoa alisema, hifadhi
hizo zina changamoto nyingi sana hasa suala la kuingiza ng’ombe ndani ya Mapori
hayo. Aidha Uongozi wa Mkoa unajitahidi kufanya operesheni za kuondoa mifugo
kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Hifadhi za Taifa
(TANAPA), Wakala wa Huduma za misitu(TFS), na Mamlaka ya Usimamizi wanyamapori
Tanzania (TAWA). Mfano amezungumzia
operesheni ya hivi karibuni iliyofanyika katika Hifadhi za Jumuhiya ya jamii za Wanyamapori
(WMA) kwa kuondoa mifugo, na kuchoma nyumba za makazi zaidi ya 1,069
zimevunjwa.Akizungumzia Bonde la Mto Kilombero, amesema vilevile amefanya
operesheni ya kuondoa mifugo katika Bonde la Kilombero .
Mhe. Japhet Ngailonga Hasunge (Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii) |
Dkt.Stephene
Kabwe (Kulia) akimueleza jambo Naibu Waziri mbele ya watumishi wa TAWA na Mkuu
wa Mkoa ofisini kwake Morogoro.
|
Dkt.KJames Wakibara(wa nne kushoto), Bw.Edgar Masunga (wa tatu kutoka kushoto), Bw.Kaisi Mwaikambo (wa pili kushoto) na Bw. David Kanyatta (wa Kwanzaa kushoto) |
Naibu waziri asifu
juhudi zinazofanywa na Mkoa wa Morogoro katika kukabiliana na changamoto
mbalimbali za uhifadhi. Pia alimshukuru Mhe. Rais kwa kumteua kushika nafasio
hiyo. Alimueleza Mkuu wa Mkoa kuwa Wizara ya Malaisili na Utalii ina majukumu
ya kutangaza utalii wa ndani na nje ya nchi, kuhakikisha raslimari za
wanyamapori zinalindwa,na amesemaWizara inajikita kujitangaza zaidi utalii wa
kusini mwa Tanzania.
Naibu waziri baada ya kusalimiana na Mkuu wa Mkoa alitembelea ofisi za
TAWA Makao Makuu na kusaini kitabu cha wageni na baadaye kuongea na watumishi.
Kabla ya kuanza hotuba yake alikaribishwa na Dkt. James Wakibara (Kaimu
mkurugenzi Mkuu-TAWA) kwa kumueleze mambo machache kuhusu TAWA.
Naibu Waziri akisalimiana na Bw. Chuwa (Afisa Malaisili wa Mkoa wa Morogoro) mbele ya Ofisi za Makao Makuu ya TAWA na pembeni Mkurugenzi Mkuu-TAWA akishuhudia |
phor
Naibu Waziri akiwa na Mkurugenzi wa TAWA ofisini kwake |
Dkt Wakibara alisema’ Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania (TAWA) ni mamlaka iliyoanzishwa kwa Amri ya Serikali na
kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Na.135 la tarehe 9 Mei, 2014. Uanzishwaji
wa Mamlaka hii ni utekelezaji wa kifungu cha 8 cha Sheria ya kuhifadhi
Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009’.
Dkt.James
Wakibara (Mkurugenzi Mkuu-TAWA) akifikiria jambo kwa makini
Dkt Wakibara alitaja malengo makuu ya TAWA:-
i.
Kuboresha usimamizi wa raslimari za wanyamaspori nje
ya hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
ii.
Kuimarisha usimamizi wa wanyamapori
iii.
Kuboresha ubora na ufanisi wa utendaji kazi
Dkt wakibara
alimueleza Naibu waziri kwa kutaja maeneo yanayosimamiwa na TAWA kuwa ni:-
·
Mapori ya Aiba 28 (114,782 km2)
·
Mapori tengefu 42 (56,765 km2)
·
Maeneo ya Ardhioevu (3) (48,634 km2)
Dkt Wakibara
kuhusu masuala ya utalii alimueleza Naibu Waziri kuwa TAWA inasimamiwa vitalu
vya uwindaji157, ingawa vinachangamoto, vitalu 61 viko wazi; 24 havikupata
wawekezaji;47 vilirejeshwa; 54 vimetangazwa upya mwezi Septemba,2017.
Kuhusu suala
la ujangili, Dkt.Wakibara alimueleza
Naibu Waziri kuwa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika kukabiliana na
ujangili na kutoa takwimu ambazo TAWA imefanya tangu kuanzishwa kama
ifuatavyo:-
a.
Siku doria 58,580 (66%) zimefanyika
b.
Siraha 112 zilikamatwa zikiwepo SMg 2, Rifle 9 Shotgun
22, Bastola 2, Gobore 87, fataki 54, Risasi 985
c.
Watuhumiwa 889 walikamatwa, kesi 415 zimefunguliwa
d.
Wanyama waharibifu siku doria 4,820 ongezeko la 53.4%,
matukio 160.
Akizungumzia
mifugo,alimueleza kuwa jumla 14,059 ilikamatwa
·
Ng’ombe 13,865; mbuzi94; punda33; kondo67
·
Mifugo 2,121 iliuzwa kwa amri ya mahakama
·
Mifugo 11,938inaendelewa kushikiliwa
·
Mapori sugu ya mifugo;Maswa,BBK,Moyowosi/Kigosi,
Rungwa/Kizigo/Muhesi,Uwanda, Selous,Ikorongo/Grumeti, Swagaswaga, Mkungunero na
Kilombero GCA.
Kuhusu
utengenezaji mipaka wa mipaka, jumla ya vigingi 799 viliwekwa katika maeneo
mbalimbali. Katika Mapori ya Akiba 20.
(hadi sasa 40%)
Baada
ya Hotuba ya Dkt. James Wakibara, alimueleza Naibu Waziri mbali na changamoto
mbalimbali za uhifadhi, TAWA imefanikiwa kuongeza mapato yake kutoka Bill 36
hadi 38 kwa mwaka.
Naibu Waziri akizungumza na watumishi,
alisistiza mambo yafuatayo katika hotuba yake:-
i.
Aliwashukuru uongozi mzima wa TAWA kwa kazi nzuri za kupambana na ujangili na kulinda raslimari za wanyamapori
ii. Aliwaomba TAWA waongeze mapato kwa kutumia mfumo wa kielekroniki
iii. Aliwapongeza TAWA kwa kujadili na kuandaa Mpango mkakati wa TAWA (Strategic Plan) ambayo iko kwenye hatua za mwisho kumalizika
iv. Amewaomba TAWA kuongeza juhudi za kuanda Sheria ya TAWA ipatikane haraka iwezekanavyo
v. Matarajio ya Serikali ya awamu ya tano ni kuchapa kazi na kwa uadilifu na kuepukana navitendo vya rushwa.
vi. Amewaomba watumishi kuwa wabunifu
vii. Amewaomba watumishi kudhibiti mifugo yote inayoingia Mapori ya Akiba na maeneo mengine ya uhifadhi kwa kufuata sheria. Mifugo yote iondolewe ndani ya hifadhi.
viii. Amesisitiza kuwa Wizara inaweka msisitizo wa jeshi husu kwenye Taasis zake zote
ix. Utoaji wa Elimu kwa wananchi, shuleni,vyuo ni kitu muhimu, waelimishwe kwa njia za mikutano,redio,Tv, vpeperushi na Maonesho ya sinema
x. Aidha ,amesisitiza TAWA waongeze kasi ya kujitangaza hasa masuala ya Utalii
xi. Kufahamishana habari mbalimbali za utendaji (Sharing Information) ni kitu nyeti
Aliwashukuru uongozi mzima wa TAWA kwa kazi nzuri za kupambana na ujangili na kulinda raslimari za wanyamapori
ii. Aliwaomba TAWA waongeze mapato kwa kutumia mfumo wa kielekroniki
iii. Aliwapongeza TAWA kwa kujadili na kuandaa Mpango mkakati wa TAWA (Strategic Plan) ambayo iko kwenye hatua za mwisho kumalizika
iv. Amewaomba TAWA kuongeza juhudi za kuanda Sheria ya TAWA ipatikane haraka iwezekanavyo
v. Matarajio ya Serikali ya awamu ya tano ni kuchapa kazi na kwa uadilifu na kuepukana navitendo vya rushwa.
vi. Amewaomba watumishi kuwa wabunifu
vii. Amewaomba watumishi kudhibiti mifugo yote inayoingia Mapori ya Akiba na maeneo mengine ya uhifadhi kwa kufuata sheria. Mifugo yote iondolewe ndani ya hifadhi.
viii. Amesisitiza kuwa Wizara inaweka msisitizo wa jeshi husu kwenye Taasis zake zote
ix. Utoaji wa Elimu kwa wananchi, shuleni,vyuo ni kitu muhimu, waelimishwe kwa njia za mikutano,redio,Tv, vpeperushi na Maonesho ya sinema
x. Aidha ,amesisitiza TAWA waongeze kasi ya kujitangaza hasa masuala ya Utalii
xi. Kufahamishana habari mbalimbali za utendaji (Sharing Information) ni kitu nyeti
Naibu waziri akikaribishwa na Dkt.Felician Kirahama(M/Kiti wa Bodi ya TAFORI) alipowasili kuongea na watumishi wa TAWA. |
Baadhi
ya watumishi wa TAWA wakimsiliza Naibu Waziri (Hayupo kwenye picha hii)
|
Watumishi wa TAWA wakimsikiliza |
Bw.Mabula
Misungwi (Kaimu Mkurugenzi Huduma za ulinzi wanyamapori-TAWA).
Bw.Nkuwi Richard (Kaimu Mkurugenzi Huduma za Utalii na Biashara-TAWA) |
Bw.David Kanyatta (Kaimu Mkurugenzi huduma za raslimari wanyanyamapori-TAWA) wa kushoto. |
Bw.Willian Kitebi (Kaimu Mkurugenzi Huduma za TAWA) |
Imeandaliwa
na,
Twaha Twaibu
AFISA
HABARI NA MAHUSIANO-TAWA
No comments:
Post a Comment