Meneja Peacock mbaroni kwa ushoga..Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abraham Ntambara
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Peacoak kwa kosa
la kuhifadhi watu 12 wanaodaiwa kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja (Ushoga).
Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Lazaro Mambosasa akizungumza na waandisi wa habari.
Watu hao ni raia wa Afrika Kusini wawili, Uganda mmoja na Tanzania tisa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaan Kamanda wa Kanda hiyo,
ACP Lazaro Mambosasa amesema sheria za nchi zinakataza vitendo vya ushoga na ni kinyume cha
utamaduni.
“Kitendo cha kuhamasisha kuingiliana kinyume na maumbile ni
kosa la kisheria, vitendo hivyo vya ushoga haviruhusiwi nchini,” amesema ACP
Mambosasa.
Amesema mwananchi yeyote Dar es Salaam atakaye hifadhi
watu wa jinsi hiyo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Wakati huo huo Jeshi hilo limefanikiwa kukamata Silaha aina
ya SMG, Bastola moja aina ya CZ Magazine mbili, risasi 17, Mabomu aina ya
Graned saba, pikipiki moja aina Ferkon
na kuuwa majambazi watano wasiotambulika majina.
Katika hatua nyingine, Kamanda Mambosasa ameeleza kupatikana
kwa magari ya wizi, vitu mbalimbali vikiwemo laptop 3, simu 100 na kukamatwa
kwa watuhumiwa tisa wa wizi huo.
ACP Lazaro Mambosasa akionyesha waandishi wa habari Mabomu aina ya Graned waliyokamata.
No comments:
Post a Comment