Waziri Mpina apiga marufuku mnada wa mifugo...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amepiga marufuku kupigwa mnada mifugo inayokamatwa kwenye hifadhi mbalimbali nchini bila maafisa mifugo kuipima na kujiridhisha kama haina magonjwa.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amepiga marufuku kupigwa mnada mifugo inayokamatwa kwenye hifadhi mbalimbali nchini bila maafisa mifugo kuipima na kujiridhisha kama haina magonjwa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
Marufuku hiyo ameipiga leo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma
aliposhiriki katika zoezi la ukamataji wa mifugo Zaidi ya 170 iliyoingia kutoka
nchi jirani ya Rwanda.
Amesema “ili kuepuka kuenea kwa magonjwa ya wanyama hao
sambamba na kuwachukulia hatua kali wananchi ambao wamekuwa wakipokea na kubeba
dhamana ya mifugo kutoka nje ya nchi huku wakidai kuwa ni ya kwao,”.
Aidha amebainisha kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na
amewataka wafugaji wanapokamatiwa mifugo yao wajitokeze mara moja ili kuepuka
usumbufu unaojitokeza.
Waziri Mpina amesema serikali itaendelea kuwachukulia hatua
kali wananchi ambao wamekuwa wakipokea na kukubali kubeba dhamana ya mifugo
kutoka nje ya nchi huku wakidai kuwa ni ya kwao
No comments:
Post a Comment