Kesi ya uchochezi ya Lema kusikilizwa kwa siku 3 mfululizo..Soma habari kamili na Matukio360..#share

KESI ya Uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demkrasia na Mendeleo (Chadema) Godbless Lema inatarajiwa kusikilizwa mfululizo kwa siku tatu katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha.
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema

Hayo yemebainishwa leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Devota Msoffe, amesema kutokana na kesi hiyo kuwa nje ya wakati, itasikilizwa kuanzia Novemba 27 hadi 29, 2017 ambapo upande wa Jamhuri ndiyo utakaoanza kuleta mashahidi wao.

“Tutasikiliza kesi hii siku tatu mfululizo kwani iko nje ya wakati na natoa agizo kwa mashahidi wa Jamhuri kuitwa ambapo tunatarajia kufunga ushahidi wao Novemba 29,” alisema Hakimu huyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya jana upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa huyo ambaye pia anakabiliwa na kesi nyingine ya uchochezi katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.



Wakili wa Serikali, Agness Hyera, akimsomea Lema maelezo ya awali katika kesi hiyo namba 440 ya mwaka 2016, alidai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na shtaka moja la uchochezi  ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 22, mwaka jana katika eneo la Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro akiwa anahutubia mkutano wa hadhara.

Miongoni mwa maneno ya uchochezi anayodaiwa kuyatoa Lema ni pamoja na: “Rais Magufuli akiendelea na tabia ya kudhalilisha demokrasia na uongozi wa upinzani iko siku Taifa litaingia kwenye umwagaji wa damu,…. “Rais yeyote ambaye haheshimu mipaka ya sheria, mipaka ya Katiba, rais huyo ataliingiza Taifa katika majanga na umwagaji damu,watu watajaa vifua, wakiamua kulipuka polisi hawa wala jeshi halitaweza kudhibiti uhalifu utakaojitokeza.”

Baada ya kumsomea mashtaka hayo, Wakili Hyera aliiomba mahakama kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza na kuwa hawakuwa tayari kuweka hadharani majina ya mashahidi wao wala vielelezo ambapo alisema wanatarajia kuwa na mashahidi wasiozidi 10.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search