Zitto amvaa Samson Mwigamba...Soma habari kamili na Matukio360...#share
KIONG0ZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama chake siyo jukwaa la kuisifia Serikali kama wanachama wengine wanavyodhani.
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe.
Aidha amweataka wanachama ambao wanaona chama hicho kimewashinda wajiondoe wenyewe bila kukipaka matope Chama hicho kwani hakijaacha misingi yake kama baadhi ya wanachama wanavyotuhumu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Zitto amesema wanachama wanaodhani kama chama hicho ni jukwaa la kuisifia Serikali wajitathimini au kuchukua hatua kama wenzao walivyofanya.
Zitto amesema hayo ikiwa ni siku chache tangu aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba na wenzake kuhamia Chama cha Mapinduzi ( CCM) kwa madai kuwa ni kuiunga mkono serikali katika kitetea maslahi ya wananchi wanyonge pamoja na kupiga vita rushwa.
“Tulimwita Mwigamba katika kikao cha chama aje kutueleza kama tunakikuka misingi ya chama lakini hakufika. Chama kinaheshimu mchango wa kila Mwana-ACT, lakini tunawashauri wanaondoka wasiwashawishi wanachama wengine kuondoka,” amebainisha.
“Chama kimejiridhisha kwamba bado tunaendelea kusimamia misingi ikiwamo uzalendo sanjari na kupigania haki za demokrasia,”amesema Zitto.
Amesema wanafanya yote hayo wakiongozwa na utu na uadilifu.
“Chama chetu kina ahadi tano ambazo ni kupambana na rushwa na ufisadi na kamati ya uongozi imebaini kama haijatoka katika misingi yake kama wengine wanaoondoka wanavyodai,”amesema Zitto.
Amesema bado wanaendelea kupambana na umasikini na hali ya maisha kwa Watanzania wote.
“Hatujawahi hata siku moja kwenda kinyume na misingi ya chama hiki kama watu wanavyodai.”
No comments:
Post a Comment