Kesi ya Lulu dhidi ya Kanumba ushahidi wa mke Dk Slaa wasomwa..soma habari kamili na Matukio360..#share

Na Mwandishi wetu
 MAELEZO ya ushahidi wa Josephine Mushumbus ambaye ni mke wa Dk Willbrod Slaa katika kesi ya mauaji inayomkabili Lulu, yamesomwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania na mstaafu Sajenti Detective, E 103 Nyange (53)
Msanii wa filamu, Elizabeth Michael'Lulu'

Maelezo hayo yamesomwa baada ya wakili wa utetezi, Peter Kibatala kumueleza Jaji Sam Rumanyika kuwa wanaomba askari huyo ayasome maelezo ya Mshumbus ambaye ni shahidi wao wa pili kwa sababu yeye ndiye aliyemuandikia.

Akisoma maelezo hayo, amesema anamfahamu Mushumbus na ndiye aliyeandika maelezo yake ya ushahidi.

Amesema  katika maelezo hayo Mushumbus amejitambulisha kuwa ni Daktari, ana miaka (46) Mkazi Bunju National Housing na aliyaandika maelezo hayo April 23/2012.

Akimnukuu Mushumbus, askari huyo alisoma kuwa;Nasema kwamba mimi ndio mwenye jina la Josephine S Mushumbus , pia ni mmiliki wa kituo cha Tiba Mbadala cha Precious kilichopo maeneo ya Mawasiliano Tower (Sam Nujoma).

Nina wateja wengi wa umri tofauti, mmoja wa wateja wangu ni Steven Kanumba ambaye kwa sasa ni marehemu. Nakumbuka August 2011 ndio nilimfahamu Kanumba ambapo alikuja akiwa na tatizo akitaka nimtoe sumu katika mwili wake. Kuanzia hapo akawa anakuja katika kliniki yangu mara kwa mara kwa ajili ya huduma hiyo.

Kila alipokuja nilikuwa nampima kwa kutumia mashine ya kutolea sumu ambapo kwa kufanya hivyo niligundua ana mafuta ( cholesterol) na tatizo la moyo.

Pia alikuwa na upungufu wa hewa katika ubongo wake ambapo hali hiyo ilimletea udhahifu katika mwili.

Mfano alikuwa na tatizo la maumivu ya moyo mara kwa mara, ubongo na akili ilichoka.

Katika kumuhudumia niligundua anafanya mazoezi ya kutanua misuli mara kwa mara ambapo nilimwambia aache kwa sababu mfumo wake wa damu sio mzuri, hivyo anaweza kusababisha kifo.

Kama kujua mtu kafa kwa kukosa hewa, misuli yake akifa inakuwa na rangi ya Blue.

Pia aliwahi kunambia ana matatizo makali ya moyo ila hakunambia yanasababishwa na nini, hivyo akaniomba ushauri nasaha.

Hivyo tulipanga appointment kwa ajili ya kumpa ushauri nasaha ila siku chache baadae nikasikia amefariki dunia.

Baada ya kusoma maelezo hayo, aliiomba mahakama iyapokee kama kielelezo ambapo mahakama ilikikubali.

Hata hivyo, upande wa mashtaka kupitia Wakili Faraja George uliiomba mahakama imtambue askari huyo kama shahidi na sio msomaji maelezo ya Mushumbus.

Kutokana na mvutano wa kisheria Jaji Rumanyika alitoa uamuzi ambapo alisema askari huyo atatumbulika kama shahidi.

Wakili Kibatala akaieleza mahakama kuwa wamefunga ushahidi wao.

Kutokana na hatua hiyo, Jaji Rumanyika amesema Oktoba 26/2017 atatarajia kupata maoni kutoka kwa Baraza la Wazee, kabla ya kutolewa hukumu ya kesi hiyo

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search