ACT Wazalendo wamkosoa rais Magufuli katika mambo tisa....soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeainisha mambo tisa ambayo Serikali
ya awamu ya tano imefanya vibaya katika
miaka miwili ya uongozi wa Rais John Magufuli.
Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Yeremia Maganja.
Mwenyekiti wa chama hicho, Yeremia Maganja, akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema mambo hayo
yamegawanywa katika mafungu makuu matatu.
“Leo tutatoa tathmini yetu ya miaka miwili ya utawala huu,
tathmini hii ni zao la utafiti husika uliofanyika nchi nzima. Tathmini yetu
itaainisha mambo 9 ambayo tunaamini hayakufanywa vizuri kabisa na Serikali,”
amesema Maganja.
“ACT Wazalendo inao wajibu wa kujihusisha na masuala ya watu,
tunatimiza wajibu huo kwa tathmini hii ya kuangazia mambo haya risa ambayo ni
mapungufu ndani ya miaka miwili hii ya utawala huu,”ameongeza.
Amesema mambo hayo yamefanya vibaya kiasi cha kuleta athari
nchini, kisiasa, kiutawala na kiuchumi.
Ametaja maeneo hayo kuwa ni ya, Haki za Msingi Usimamizi wa Uchumi na Uendeshaji wa Nchi.
Haki za Msingi
Maganja amesema kumekuwepo
na uminywaji wa uhuru wa Vyama vya Siasa Kufanya mikutano ya hadhara, uhuru wa
Vyombo vya habari, pamoja na Uhuru wa Kujieleza, Kuminywa kwa haki ya
wazanzibari kuchagua viongozi wao na Kupuuzwa kwa matakwa ya Katiba Mpya.
Usimamizi wa Uchumi wa
Nchi
Amesema kumekuwepo kwa hali ya Kusinyaa kwa Uchumi wa Nchi,
Kudhohofishwa kwa Sekta Binafsi,
Mazingira Mabaya ya Biashara Nchini, pamoja Kupaa kwa Deni la Taif.
Mengine ni kutelekezwa kwa kilimo na utekelezaji wa miradi
mikubwa bila kuzingatia maslahi ya umma.
Uendeshaji wa nchi
Mwenyekiti huyo amesema
katika kipengele hiki serikali hii imefanya vibaya kwa uvunjaji wa misingi ya
Sera ya Mambo ya Nje, unyanyasaji wa watumishi wa umma na utawala unaovunja taasisi
za kikatiba na kisheria kutoakana na kwamba utawala huu umekuwa wa mtu mmoja.
No comments:
Post a Comment