Tanzania kutoa tuzo za Pan African....soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abraham Ntambara
RAIS na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kimataifa
wa masuala ya kidiplomasia na maendeleo ya kijamii.
Katikati ni mratibu wa mkutano wa kimataifa wa masuala ya kidiplomasia na maenedeleo ya kijamii kutoka YUNA, Selemani Kitenge.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Novemba 18, 2017 jijini Dar
es Salaam. Pamona na mambo mengine kutatolewa tuzo kwa mashirika na wadau mbali
mbali, tuzo hizo zinajuliakana kama Pan African Humanitarian Summit and
Awards 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Mkutano huo
Selemani Kitenge kutoka Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa nchini (YUNA), amesema Tanzania imepewa heshima kwa mara ya
kwanza kuandaa mkutano huo.
“Dhumuni la mkutano huu ni kutambua jitihada mbali mbali
zinazofanywa na wadau barani Afrika ili kuendeleza na kudumisha amani na
maendeleo ya Afrika,” amesema Kitenge.
Aidha amesema mkutano huo utawaleta pamoja wanadiplomasia,
wadau wa maendeleo, vijana madhubuti kutoka nyanja mbali mbali barani Afrika na
viongozi wa serikali ili kuajdili mustakabali wa dhima kuu ya mkutano wa mwaka
huu utabebwa na kauli mbiu ya ya ‘Amani inewezekana Jana, Sasa na Kesho’.
Kitenge alitaja vipengele viwili muhimu katika tuzo hizo kuwa ni Rafiki wa
Afrika, tuzo ambazo watapewa watu wasio wakazi wa bara la Afrika ambao wamekuwa
wakichangia maendeleo barani humu.
Amesema kipengele kingine ni tuzo ya Ujenzi wa Taifa na Amani
ambayo watapewa watu wenye mchango katika ujenzi wa amani barani Afrika.
Pan African Humanitarian Summit and Awards zilianza toka
mwaka 2015 na kufanyika nchini Ghana na mwaka 2016 zilifanyika nchini Dubai.
Tanzania inakuwa nchi ya pili Afrika kuandaa mkutano huu.
No comments:
Post a Comment