BAKWATA:Sensa si mfarakano...soma habari kamilli na Matukio360..#share
Salha Mohamed
UMOJA wa Vijana wa Baraza
Kuu la Waislamu Taifa (Bakwata), limewatoa hofu waislamu wanaodhani mchakato wa
sensa kwa waislamu ni chanzo cha mfarakano wa taifa.
Katibu Umoja wa Vijana wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Othman Zuberi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa tamko la kumpongeza na kumuunga mkono utendaji kazi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa jijini Dar es
Salaam na Katibu wa Umoja huo, Sheikh Othman Zuberi wakati wa kutoa tamko la
pongezi na kuunga mkono utendaji kazi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar
Zuberi katika kipindi cha miaka miwili.
Amesema sensa kwa maendeleo
ya waislamu inafaa jambo linaloonesha umakini wa kuwatumikia waislamu na kutoa
huduma kwa usahihi kwa watu anaowatumikia.
"Hivi karibuni Mufti
aliwaagiza makatibu wa Baraza kujiandaa na sensa ya waislamu, msikiti na
madrasa kote nchini, "amesema.
Amewatoa hofu vijana nchini wanaoona mchakato huo unaweza kuwa
chanzo cha mfarakano wa taifa kiimani.
" Hasha wa kala haiwezi
kuwa hivyo kwani tunavyomfahamu Mufti ni mwenye kuongoza na qur-an na hadithi
za mtume vyanzo ambavyo vimejaa mahimizo ya mshikamano,"amesema.
Ameongeza kuwa kufanya sensa
kwa waislamu ni ibada huku akisisitiza haiwezi kuwa chanzo cha mfarakano baina
yao na kwamba inaleta maendeleo kwa waislamu.
Amesema katika kipindi cha
miaka miwili, Mufti amefanikiwa kupata wahisani wa kujenga ofisi za kisasa za
Bakwata na kuonesha ushirikiano baina ya waislamu na waislamu waislamu pamoja
na waislamu na wasiokuwa waislamu.
"Tulizoea kuona
mafarakano na kashfa za wazi baina ya makundi lakini sasa yamepungua kwa kiasi
kikubwa au hayapo kabisa, "amesema.
Ameziomba taasisi za dini
nchini kumuunga mkono Mufti katika mema anayoyafanya kwa maslahi ya waislamu na
taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment