Bwakata yaendelea kusaka mali za waislam kimya kimya...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Salha Mohamed
SHEIKH
Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi anaendelea kufuatilia mali za waislamu kimya
kimya ili aweze kufanikiwa kuzipata.
Katibu Umoja wa Vijana wa
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Othman Zuberi akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa tamko la kumpongeza na
kumuunga mkono utendaji kazi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi
leo jijini Dar es Salaam.
Hayo
yameelezwa leo Dar es Salaam na Katibu wa Umoja wa Vijana Bakwata Taifa,
Sheikh Othman Zuberi wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema
tangu Sheikh Zuberi alipochaguliwa Septemba 10,2015 alianza msako wa mali za
waislamu. Amesema
waislamu waondoe wasiwasi mali zao kwani muda si mrefu matunda ya mali hizo
yataonekana.
"Akiwa
na muda mfupi mno tangu alipochaguliwa, Mufti alianza msako wa mali za waislamu
jambo ambalo analifuatilia kwa umakini na uangalizi wa hali ya juu,
"amesema.
Amesema
muda si mrefu waislamu wataanza kuona matunda yake kwani anafuatilia kimya
kimya na kwa umakini.
"
Utaratibu wa urejeshaji wa mali za Baraza zilizopotea unaendelea kufanyika, baraza
limefanya ukaguzi na uboreshaji wa shule, kuanzisha daaru (maarif ya kujifunzia
elimu zote za dini, kusimamia sera ya
mahusiano mazuri baina ya waislamu, "amesema.
No comments:
Post a Comment