Kigamboni marathon Disemba 2, 2017...Soma habari kamili na Matukio360..#share
KATIKA jitihada za kuijengea Jamii uelewa na hamasa juu
ya umuhimu wa kutunza afya na Kufanya Mazoezi, Kampuni ya
Events World kwa kushirikiana na wadau
mbali mbali imeandaa mbio za ‘Kigamboni Marathon’ zinazotarajia kufanyika Disemba 2, 2017.
Mratibu Mwenza wa Shindano la Kigamboni Marathoni,Dimo Debwe Mitiki
akiwaonesha wana Habari Zawadi zitakazogawiwa kwa washindi wa mbio hizo
zinazotarajiwa kufanyika Desemba 2 mwaka huu katika fukwe za Kigamboni jijini
Dar es Salaaam
Mbio hizo zitaambatana na zoezi la Upimaji wa afya katika
kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo huazimishwa Desemba 1 ya kila mwaka.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi
wa kampuni Events World Dimo Mitiki, amesema lengokuu la mbio
hizo ni kutangaza fursa za uwekezaji, vivutio
vya kitalii na biashara zilizopo Kigamboni kwa maendeleo ya Taifa letu.
Aidha ameongeza kuwa zinafanyika ili kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan katika kuhamasisha Watanzania kufanya mazoezi
ili kuimarisha afya.
“Pia kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia viongozi wetu
wakihamasisha wafanyabiashara na wadau mbali kuwekeza ndani ya wilaya yetu mpya
ya Kigamboni, hivyo ni imani yetu kuwa kufanyika kwa ‘Kigamboni Marathon’
kutawavutia watu mbali mbali kufika Kigamboni na kujionea uzuri pamoja na fursa
zilizopo kigamboni,” amesema Mitiki.
Naye Mratibu wa mbio hizo Juma
Mtetwa amesema kuwa Kigamboni imezungukwa na maeneo mazuri ya kimichezo,
Utalii na Uwekezaji kuliko sehemu yeyote Jijini Dar es saalam.
Amesema, hiyo ni sababu moja wapo inayowasukuma kuamini kuwa
‘Kigamboni Marathon’ itakuwa ni miongoni mwa mbio bora zaidi nchini itakayoibua
wakimbiaji wazuri watakao leta ushindani mkubwa katika mchezo huu wa riadha
Duniani kote.
“Kigamboni Marathon inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya mji
mwema jirani na ofisi za Halmashauri mpya ya kigamboni Disemba 2, 2017,
kutakuwa na mbio za urefu wa kilomita 21(Half Marathon), kilomita 10 na mbio
kwaajili ya watoto, wazee na hata wale wasio na mazoezi ya mara kwa mara (Fun
Run) pia zawadi mbali mbali kushindaniwa zikiwemo Medali za dhahabu, Silver na
gold pia pesa taslimu kwa washindi,” amesema.
Kwa niaba ya Kamati ya maandalizi ya ‘kigamboni Marathon’ amewashukuru wadau wote waliojitokeza kuunga mkono katika Jambo
hili lenye tija kwa Maendeleo ya Taifa wakiwemo viongozi wa ndani na nje
ya Kigamboni, wanahabari, taasisi mbali mbali, kampuni na jamii.
Pia alizishukuru kampuni zilizojitokeza kudhamini mbio hizo
ikiwemo Property International, Itel Mobile, Coca cola kupitia kinywaji cha
Dasani, J.P.M Hospital, Akemi Restaurant, PCMC Hospital na Red Bull na kuomba
wadau na makampumi mbali mbali kujitokeza na ku- support mbio hizo.
Amesema ushiriki wa kampuni kubwa kutoka ndani na nje ya
Kigamboni unatoa fursa kwa wafanyabiashara waliyopo Kigamboni na amewasihi
wanakigamboni kuitumia fursa hiyo kujumuika pamoja na kuonyesha walichonacho
lakini pia kufahamiana na kuongeza Marafiki wenye tija.
Aidha amewakaribisha kuwakaribisha wadhamini, washiriki
na wadau mbalimbali kuhudhuria katika tukio hilo la kipekee.
No comments:
Post a Comment