Dk Shika kuunguruma Desemba 9...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Hussein Ndubikile
‘BILIONEA’ wa nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi, Dk Luis
Shika anatarajia kutoa simulizi ya maisha yake katika hafla maalum ya usiku wa
900 itapendeza itakayofanyika Desemba 9, 2017.
Meneja wa Dk Luis Shika, Catherine Kahabi katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa, wa kwanza kulia ni Dk. Shika na kwanza kushoto meneja burudani Rajab Mteta.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Meneja wa dokta
huyo, Catherine Kahabi wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na hafla
hiyo.
"Dk. Shika ataongea historia yake alipotoka na mpaka
alipo pia kutakuwepo burudani kwa wananchi watakaohudhuria," amesema.
Amesema lengo la hafla hiyo ni kumtambulisha Dk. Shika kama
miongoni mwa watu walioupata umaarufu kwa muda mfupi, kumpongeza kwa kushinda
mnada wa nyumba za tajiri Lugumi na kumuweka rasmi kwenye muonekano wa u
bilionea.
Catherine amesema katika tukio hilo mgeni rasmi anatarajia
kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrence Mashi na itahudhuriwa na watu zaidi
ya 5,000.
Kwa upande wake, Dk Shika amewaomba wananchi kujitokeza kwa
wingi kusikiliza mambo mengi atakayoyaongea kuhusiana na historia yake.
Naye Meneja Burudani wa ukumbi huo, Rajab Mteta amesema hafla
hiyo itasindikizwa na bendi mbalimbali ikiwemo Twanga Pepeta, Jahazi Modern
Taarab, wasanii wa Bongo Fleva akiwemo Juma Nature pamoja na mchekeshaji
maarufu, Mc Pilipili.



No comments:
Post a Comment