Hukumu mtoto wa Chacha Wangwe leo...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Abdulrahim Sadiki
HUKUMU
ya kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii inayomkabili
BOB Chacha Wangwe ambaye ni mtoto wa
mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe, itatolewa leo Novemba 15, 2017
Hukumu
hiyo inatarajiwa kutolewa na katika Mahakam aya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi siku hiyo baada ya upande wa Mashtaka kuwaita mashahidi
sita kutoka ushahidi kwenye kesi hiyo na mshtakiwa huyo kutoka utetezi wake
yeye mwenyewe.
Kwa
mujibu wa kesi hiyo namba 167, 2016
ambayo ilifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 12,2016.
Bob Chacha Wangwe ambaye kitaaluma ni mwana sheria na
mwanaharakati wa haki za binadamu anadaiwa kutenda kosa la
kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa Facebook.
Mshtakiwa
huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Machi 15,2016 na kwamba alichapicha maneno
haya; “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka
Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya
Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.”
No comments:
Post a Comment