Ilala yatekeleza miradi ya maendeleo kwa asilimia 98...soma habari kamili na Matukio360...#share

Na Husein Ndubikile
KAMATI ya Fedha na Utawala wa Halmashauri wa Manispaa ya Ilala imesema imefanikiwa kutekeleza  asilimia 98 ya miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokusudiwa kutekeleza katika awamu ya kwanza ya mwaka fedha wa 2017/2018 na kubainisha katika kipindi cha mwezi Septemba hadi Oktoba kutumia Sh bilioni 1.2 kati ya Sh bilioni 2.5 zilizotakiwa kutumika.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya fedha Manispaa ya Ilala wakikagua moja ya mradi wa maji uliopo  Segerea wilayani humo

\Miradi iliyokaguliwa ni Ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mvuleni kata ya Msongola, Ujenzi wa Barabara ya Segerea hadi Bonyokwa, Ujenzi wa Kisima na Miundombinu ya maji Mtaa wa Segerea pamoja na Jengo la DMP liliopo ndani ya maanispaa hiyo.
 
Hay0 yamesemwa leo jijini Dar es Salaam yamesemwa na Mchumi wa Manispaa hiyo, Ando Mwankuga baada ya kamati hiyo kufanya ziara ya ukaguzi ndani ya manispaa hiyo ili kubaini utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
 
Amesema katika miradi waliyoikagua wamebainia waakandarasi kuitekeleza kwa hali ya juu  na kubainisha kiasi cha fedha kilichotengwa kimetumika ipasavyo na kwamba miradi ilyobaki itakamilishwa.
 
“ Katika maeneo tuliyotembelea tumejionea wakandarasi walivyokamilisha miradi kwa zaidi ya asilimia 90 maeneo madogo ndio yaliyobaki kukamilishwa,” amesema.
 
Amesisitiza miradi ya maendeleo inachelewa kukamilika kutokana na gharama kubwa ya miradi kulinganisha na fedha zinazopatikana kwenye vyanzo vya ndani na ruzuku ya Serikali.
 
Amefafanua kuwa changamoto nyingine ni madiwani wakiwa vikaoni hutaja miradi mikubwa tofauti na kipato cha halmshauri.

Amewashukuru madiwani wa manispaa hiyo kwa kushiriki kikamilifu katika utoaji maoni pamoja na changamoto za utekelezaji wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amesema kuwa wataalamu waliokabidhiwa miradi wamefanya kazi kwa kuzingatia maadili na uadilifu na kuchangia kukamilika kwake.

Naye Diwani wa Kata ya Segerea, Edwin Mwakatobe amesema miradi iliyotekelezwa kwenye kata hiyo imetokana na fedha zilizotengwa na kutumika ipasavyo.    
Afisa Mtendaji Kata ya Msongola Enock Segesela, ameishukuru Manispaa kwa kujenga Ofisi ya Serikali za Mtaa ya Mvuleni kwani awali walikuwa wamepanga katika fremu na kulipa kodi

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search