Jakaya Kikwete: Wasanii Tanzania acheni kulialia....soma habari kamli na Matukio360...#share

Na Mwandishi wetu

RAIS mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya  Kikwete amewataka wasanii nchini kuacha kulialia na wafanye kazi zenye ubora zitakazowafanya waweza kushindana katika soko la kimataifa 


Rais mstaaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa Televisheni  inayoshughulika na masuala ya filamu za Kitanzania kwa Wasanii wa Bongo Movie JTV ambayo itapatikana kupitia king'amuzi cha StarTimes.
 
Ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye hafla ya uzinduzi wa Television mpya ya Jason ambayo itakuwa inaonyesha filamu za kitanzania.

“Ni wakati muafaka sasa kwa wasanii kuacha kulia lia kutaka serikali iwape msadaa, badala yake mfanye  kazi zenye ubora zaidi,” amesema na kuongeza

“Msilalamike tu, mkitaka mtoke lazima  mfanye kazi nzuri itakayovuka mipaka ya Tanazania.” 



Rais Kikwete amesema ili kufukia hapo ni lazima waweze kuzalisha filamu nzuri..

Pamoja na hayo Jakaya Kikwete amesema amefurahishwa na muenendo wa tasnia ya sanaa ya filamu, ambayo kwa sasa imetoa ajira kwa watu milioni 6.


Kwa upende mwingine Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yao ya StarTimes walitumia fursa hiyo pia kutangaza kifurushi kipya cha UHURU kwa wateja wake wa antenna.

Akiongea katika hafla hiyo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo  Juma Suluhu amesema, “Imekuwa ni shauku yetu siku zote kutoa huduma ya kiwango bora kwa Watanzania na kwa gharama nafuu kabisa, kifurushi kipya cha UHURU ni ushahidi tosha na tuna hamu ya kuona wateja wetu pendwa wakikitumia na kufurahia huduma hii.”

“Tumejitolea kuwaletea huduma bora na kiwango cha juu kabisa, na maono yetu ni kuhakikisha kila familia ya kitanzania inafurahia huduma za kidigitali na maisha ya kidigitali, hivyo kila tunachofanya ni kujaribu kutusogeza katika lengo letu hilo na kifurushi kipya cha UHURU ni hatua kubwa sana.” ameongeza.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search