Serikali yateketeza makazi kwa milioni 80...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na mwandishi wetu
SERIKALI wilayani Chunya mkoani Mbeya imetumia
milioni 80 katika operesheni ya kuwaondoa
na kuteketeza makazi ya wakulima na wafugaji waliovamia kwenye maeneo ya hifadhi na misitu ya asili katika tarafa
ya Kipembawe kata ya Kambi katoto.
Baadhi ya nyumba zilizoteketezwa
katika zoezi la kuwaondoa wavamizi waliojenga makazi katika maeneo ya hifadhi
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Chunya, Rehema
Madusa alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa operesheni iliyofanyika kwa siku kumi, kuanzia
Oktoba 7, 2017 katika kikao cha kawaida cha wilaya(DCC) kilichohusisha watendaji wa
ngazi za kata, vijiji na wakuu wa idara.
Pia kilijadili sekta ya elimu, kilimo na uwekezaji wa
viwanda.
Madusa amesema kaya 18,000 zenye wakazi 9,000
ziliteketezwa na wamelazimika kufanya
hivyo kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira uliofanywa hususan ukataji miti
,uchomaji na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji na kusababisha wanyama kukimbia kwenye
hifadhi.
"Uharibifu ni mkubwa hasa kwenye maeneo wanayoishi na katikati ya hifadhi. Si rahisi kutambua uharibifu huo, hakuna shule, zahanati, maji na nishati ya
umeme jambo linalosababisha watoto kukosa haki za msingi ikiwamo ya elimu
na wajawazito kujifungulia katika mazizi
ya ng'ombe "amesema.
Madusa amesema kwa sasa wamekwama kuendelea na zoezi
hilo kutokana na ukata wa fedha na ameonya watendaji kutotanguliza maslai ya
fedha kwa kuwashawishi kurejea katika
maeneo waliyoondolewa na watakaobainika watawajibishwa
kwa mujibu wa sheria.
Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo, Sophia Kumbuli
amekea tabia ya watendaji kufumbia macho wavamizi kurejea katika maeneo waliyoondolewa na watakaobainika hawatoshi kuitumikia
halmashauri hiyo.
"Nasikia chinichini kuna wakulima na wafugaji
walioondolewa wameanza kurejea tena, sasa nashangaa ninyi watendaji mko wapi
kwa kweli katika hili siwezi kuvumilia kwani serikali imetumia gharama kubwa na
nyinyi wanarejea mnawatazama hapo ni lazima kuna maslai binafsi," amesema.
Naye Ofisa Maendeleo ya jamii wilaya, Ally Ally, amesema halmashauri
inapata asilimia 65 ya mapato kutoka
katika zao la Tumbaku lakini changamoto ni uharibifu wa mazingira.
Ofisa Mtendaji Tarafa ya Kipembawe, Kassim Kirandomara
ameiomba halmashauri kutoa ushirikiano wa haraka watakapohitaji katika
zoezi la kuwaondoa wavamizi kwa kutuma askari wa jeshi la polisi
No comments:
Post a Comment