Kabla ya kuivaa Chelsea, Mourihno afikishwa mahakamani...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
mwandishi wetu
KOCHA
wa Man United Jose Mourinho amewasili katika mahakama ya Uhispania kujibu madai
ya kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa mkufunzi wa klabu ya Real Madrid.
Kocha wa Man united,Jose Mourinho
Wawakilishi
wake wamekana kuwa anadaiwa Yuro milioni 3.3 kupitia haki za matangazo ambazo
hakuzitangaza.
Mourinho
alionekana akiingia mahakamani katika makazi ya mjini Madrid Pozuelo de
Alarcon.
Kusikizwa
kwa kesi hiyo kunajiri siku moja kabla ya Manchester United kucheza dhidi dhidi
ya Chelsea katika ligi ya Uingereza siku ya Jumamosi
Mkufunzi
huyo alizungumza na vyombo vya habari siku ya Alhamisi kama ilivyo ada.
Utawala
wa Uhispania ulianzisha kesi dhidi ya Mourinho mnamo mwezi Juni.
No comments:
Post a Comment