Kikosi wachezaji wapya 'Kilimanjaro Warriors' chatangazwa...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
KOCHA Msaidizi wa timu ya taifa
za vijana 'Kilimanjaro Warriors',Oscar Mirambo ametangaza majina ya wachezaji 35 kwa ajili ya kuingia
kambini.
Kocha Msaidizi wa timu ya taifa za vijana'Kilimanjaro Warriors' Oscar Mirambo
Lengo la kambi hiyo ni kutafuta
kikosi imara cha Taifa kwa vijana wa chini ya umri wa miaka 23 maarufu kwa jina la Kilimanjaro Warriors.
Akitangaza majina
hayo Mirambo, amesema “Tunataka vijana wasiozidi 25 kwenye kikosi. Tutawapata
kwenye kambi hii ya siku 10 inayoanza Novemba 5, 2017.”
Wachezaji aliowaita
ni makipa Metacha Mnata (Azam FC), Joseph Ilunda (JKT Ruvu), Liza Mwafwea
(Tanzania Prisons).
Wengine ni Cleotas
Sospter (Yanga); Idrissa Mohammed, Bakari Kijuji (Yanga), Joseph Prosper
(Azam), Masoud Abdallah (Azam), William (Ruvu Shooting), Yussuph Mhilu (Yanga),
Adam Salamba (Stand United), Omary Mponda (Ndanda) na Stanley Angeso (Stand
United).
Pia wamo Eliud
Ambokire (Mbeya City), Emmanuel Kakuti (Mbeya City), Medson Mwakatunde (Mbeya
City), Daruweshi Shaliboko (Ashanti Unted), Abbas Kapombe (Azam/Ndanda), Ismail
Aidan (Mtibwa Sugar), Salum Kihimbwa (Mtibwa Sugar), Hassan Mganga (Mtibwa
Sugar) na Award Salum (Njombe Mji).
Wengine Awesu Ally
(Mwadui), Salum Chuku (Singida United), Yahya Zayd (Azam), Emmanuel Martin
(Yanga), Geofrey Mwashiuya (Yanga), Ayoub Masoud (Ndanda), Baraka Majogoro (Ndanda),
Mohammed Habib (Miembeni), Yussuf Mlipili (Simba), Agathon Mapunda (Njombe
Mji), Faisal Abdallah (JKU) na Yussuph Kagoma (Singida United).
No comments:
Post a Comment