Kinondoni kinara kwa wanaojiuza, bar, migogoro ya ndoa...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Salha Mohamed
MANISPAA
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ina Bar nyingi zaidi kuliko wilaya nyingine nchini,
ina migogoro 1134 ya ndoa na watu
wanaojiuza kimapenzi.
Mwenyekiti wa kamati maalum ya kurekebisha sheria za usalama barabarani, Deus Sokoni akizungumza na waandishi wa habari
Hayo
yamesemwa na Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa hiyo, Judith Kimaro katika mkutano
wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wadau kupata sera ya udhibiti wa pombe nchini
yaliyoandaliwa na Chama cha Afya ya Jamii.
Amesema
manispaa hiyo imesajili Bar 2069 na
mwaka 2016/17 imesuluhisha migogoro 76
ya watu kuacha matumizi ya pombe kupindukia iliyowasilishwa katika
manispaa hiyo.
“Madhara
ya pombe ni makubwa, tumeweza kusuluhisha migogoro 266 iliyosababishwa na pombe
iliyopindukia na watoto wengi wamebaki yatima kutokana na vifo vya wazazi wao,”amesma.
Kimaro
amesema mwaka 2016/2017 kumekuwa na kesi zipatazo 40 ambazo zipo mahakamani
zinazotokana na ubakaji na ukatili wa kijinsia kutokana na matumizi ya pombe.
Amesema
katika manispaa hiyo kuna migogoro 7 65 ya familia ambayo inaendelea
kusuluhishwa na familia 27 zimesambaratika mwaka 2016/2017.
“Kutokana
na hali hiyo, Kinondoni kumekuwa na ongezeko la watu wanaojiuza kwa jinsia zote
kama Sinza, Magomeni Kagera lakini huwa tunawatembelea na kuwashauri,”amesema.
Ameitaka
serikali kutoa elimu ya madhara ya pombe, kuweka mitaala ya madhara ya pombe
kwa ngazi ya elimu ya msingi na serikali hadi vyuo na kuweka kipaumbele katika
mapambano dhidi ya pombe kama ambavyo imeweka katika maambukizi ya Malaria na
virusi vya Ukimwi.
Mwenyekiti
wa kamati maalum ya kurekebisha sheria za usalama barabarani, Deus Sokoni
amesema kuna haja ya kurekebisha sheria ya matumizi ya pombe ili iendane na
viwango vya kimataifa.
‘Kuna
haja ya kuboresha sheria lakini tumeweka adhabu kali kwa dereva
atakayesababisha ajali tumependekeza adhabu kali kwa dereva atakayeendesha gari
akiwa amelewa adhabu iwe kuanzia sh 500,000 na kuendela,”amesema.
Amesema
Januari hadi Septemba, 2017 takribani madereva 22804 walikamatwa wakiendesha gari
wakiwa wamelewa na madereva 71 walisababisha ajali na vifo vya zaidi ya watu
300 kufariki.
Amesema
lengo hadi kufikia mwaka 2020 ni kupunguza
ajali kwa asilimia 50 na kuwa hawambembelezi dereva mlevi.
Mratibu
wa Mradi wa kupunguza matumizi ya pombe, Irene Charamila amesema mradi huo ni wa awamu ya pili umeanza 2017 hadi 2021.
“Tulifanya
utafiti kwa Wilaya za Mkuranga, Mbulu na Monduli lakini Wilaya ya Mbulu katika
Kata ya Sanubaray na Dongobesh ilionekana kuwa na matumizi makubwa ya pombe,”amesema.
Amesema
katika wilaya hiyo wanawake wanakilio cha waume zao kutumia pombe kupita kiasi
na kutohudumia familia na wanahitaji haraka sera ya udhibiti wa pombe.
Mmoja
wa wanachama hao, Daktari Geofrey Swai amesema matumizi ya pombe huaribu akili
ya mtu na kumfanya kupooza na hata kupoteza fahamu na hubadilika tabia na kutetemeka mwili anapoikosa.
“Mtu
akinywa pombe husababisha ini kukauka na kuwa na kambakamba na hatimaye
kushindwa kufanya kazi, kupata saratani ya kongosho, saratani ya mdomo,
satarani ya koromeo, kusababisha ugomvi na hata kunywa sumu,”amesema.
No comments:
Post a Comment