DPP 'amuokoa' Adam Malima...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI wa Mashtaka(DPP)
ameondoa nia ya kuendelea na kesi ya shambulio iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa
naibu waziri wa fedha katika serikali ya awamu ya nne, Adam Kighoma Malima na Ramadhani
Mohammed Kigwande
Adama Malima kushoto akitoka Mahakamani.
Kufuatia hatua hiyo Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeifuta rasmi kesi hiyo na Hakimu mkazi mkuu, Respicius Mwijage kuwaachia
huru washtakiwa hao baada ya wakili wa serikali mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa
kuomba ifutwe chini ya kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa Mashauri ya Jinai kwa
sababu Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka hayo dhidi
yao.
Kishenyi amesoma
kifungu hicho ambacho kinampa mamlaka DPP kuiondoa kesi mahakamani wakati wowote pale anapoona inafaa na pia
kinamruhusu kuirudisha mahakamani pia.
Baada
ya Kishenyi kukisoma kifungu hicho, Hakimu Mwijage alikubali na kuwaachia huru
washtakiwa wote.
Kesi
hiyo ilikuwa katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa
mashtaka.
Awali,
wakisomewa melezo ya awali (PH), Malima
na mwenzake Ramadhani Mohammed walikubali maelezo binafsi, siku ya tukio walikuwepo Masaki,
walikamatwa na kushtakiwa na wakayakana mashtaka yote yanayowakabili.
Katika
kesi hiyo, Malima anadaiwa kuwa Mei 15,2017 katika eneo la Masaki kwa makusudi
alimzuia ofisa wa polisi H.7818 PC ABDU kufanya kazi yake halali.
Malima
anadaiwa kumzuia afisa huyo kufanya
kazi yake ya kumkamata Ramadhani Kigwande kwa kosa la kumshambulia Mwita
Joseph.
Kwa
upande wa mshtakiwa wa kwanza, Ramadhani Mohammed Kigwande Naye anakabiliwa na
shtaka la kumshambulia Mwita Joseph.
Ilidaiwa
kuwa siku hiyo ya Mei 15,2017 kwenye eneo hilo la Masaki wilaya ya Kinondoni
mshtakiwa Ramadhani akiwa na nia ya
kumzuia Mwita Joseph ambaye ni afisa oparesheni wa kampuni ya Priscane Business
Enterprises wakati alipokuwa akimkamata
kwa kupaki vibaya gari namba T 587 DDL alimshambulia na kumsababishia maumivu.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo,washtakiwa wote walikana na walikuwa nje kwa dhamana kwa kila mmoja kuwa
na mdhamini mmoja ambaye alisaini bondi ya milioni 5.
No comments:
Post a Comment