Kotei:Sikuja Tanzania kutalii..Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na mwandishi wetu
KIUNGO Mghana wa Simba, James kotei amesema hakuja Tanzania
kutalii bali kufanya kazi ndiyo maana amekuwa akijituma ili kuisaidia timu hiyo
kufanya vizuri.
James Kotei
Akizungumza baada ya mchezo kati ya Simba na Mbeya City
jana, Kotei alisema kamwe hatabweteka badala yake ataendelea kupambana ili awe
bora zaidi na kutoa mchango unaohitajika kwa waajiri wake.
"Mpira ndio kazi yangu, sikuja hapa kukaa benchi, nimekuja
kucheza ndio maana namudu kucheza nafasi nyingi uwanjani.
“Nimejipanga kuisaidia Simba kufanya vizuri katika michuano ya
kimataifa mwakani,pia itakuwa fursa kwangu ya kujitangaza.
"Bado nina safari ndefu katika soka,lengo langu sio kuishia
kucheza Tanzania,nataka kusonga mbele,”alisema Kotei.
Kotei anayemudu kucheza nafasi zote za ulinzi na kiungo jana
alikuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Simba kilichoibuka na ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Mbeya City,Uwanja wa Sokoine,Mbeya.
No comments:
Post a Comment