Kocha : ‘Kilimanjaro Queens’ inakibarua kizito kutetea taji...Soma habari kamili na Matukio360..#share
NA MWANDISHI WETU
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ‘Kilimanjaro Queens’
inayotarajia kushiriki mashindano Kombe la Chalenji( Cecafa Cup)nchini Rwanda,
Sebastian Nkoma amesema Tanzania inakibarua kizito kutetea taji lao mwaka
huu.
Timu ya Kilimanjaro Queens
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Nkoma amesema ili kutetea
ubingwa wa michuano hiyo wanaoushikiria wanahitaji kufanya maandalizi ya
uhakika,lakini kinyume na hapo itawawia vigumu.
Nkoma amesema hadi sasa hajapewa muelekeo wa kambi ya timu hiyo
licha ya kuwasilisha program yake tangu Oktoba mwaka huu.
“Washiriki wengine watakaokuja kwenye mashindano hayo wamelenga
kuchukua taji ambalo sisi tunalitetea, ndio maana ninasema kutetea taji ni
shuguli ngumu kuliko kuliwania kama wenzetu watakavyokuwa wakifanya.
“Ninachofahamu mashindano haya yaliyokuwa yamepangwa kufanyika
Novemba, yamesogezwa mbele hadi Desemba ingawa tarehe rasmi haijajulikana,”amesema
Nkoma.
Nkoma amesema maandalizi ya mapema yanawasaidia wachezaji
kujipanga badala ya kukurupushwa kitu ambacho kitawafanya washindwe kufanya
vizuri.
Tanzania ilifanikiwa ubingwa ubingwa wa michuano
hiyo mwaka 2016 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya
Kenya katika mchezo wa fainali.
No comments:
Post a Comment