Mahakama yapiga marufuku 'vishoka'...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
mwandishi wetu
MAHAKAMA
imepinga vikali vitendo vya ulaghai
ikiwamo vya mawakili feki na vishoka vinavyofanywa na baadhi ya wananchi
kwa lengo la kujipatia kipato.
Ni
baada ya tukio la Jeremiah Ragita
aliyejifanya kuwa Wakili akitokea Kampuni ya Sheria ya Faithful Attorney
Advocates.
Naibu
Msajili, Mahakama ya Ardhi, Frank
Mahimbali anasema Wakili huyo feki alikamatwa mapema Novemba 8, 2017 katika Mahakama hiyo akimsimamia Mleta maombi
Nunu Mhusin Mkwata.
Mahimbali
amesema kuwa upande wa pili ambao unasimamiwa na Wakili Maros Gabriel kutoka
Kampuni ya Sheria ya 'Common Law Chambers' ulimtilia shakaJeremiah Ragita kama
kweli ni Wakili ndipo alipofanya upekuzi kwenye Ofisi ya TLS na kuambiwa kuwa
hawana jina hilo.
Hata
hivyo, Mahimbali anasema Maros alienda
mbali kwa kumuandikia barua
Msajili wa Mahakama Kuu (RHC) na kujibiwa kuwa hakuna Wakili aliyesajiliwa kwa
jina hilo.
Kwa
mujibu wa Naibu Msajili kesi hiyo ilipoitwa mbele ya Jaji Crencesia Makuru, Wakili Maros
alimueleza Jaji huyo kuwa mwenzake wa
upande wa pili sio Wakili na kisha akatoa vielelezo kutoka katika Ofisi ya
Msajili Mahakama Kuu na Ofisi ya TLS ndipo Ragita akakiri kuwa yeye si Wakili.
Hata
hivyo, Ragita alikamatwa na kupelekwa Polisi Kituo cha Kati (Central Police)
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hatua stahiki za kisheria.
No comments:
Post a Comment