Mboga mboga, matunda chanzo cha maradhi...soma habari kamili na Matukio360...#share

Na Salha Mohamed 

UTAFITI unaeleza kuwa  viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza  unaongezeka kutokana na ulaji wa mboga mboga na matunda kuwa chini ya  kiwango. 

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Neema Rugemayila, akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kisukari duniani na kampeni ya mazoezi jijini Dar es Salaam.

Utafiti huo umefanywa na Wizara y Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)  mwaka 2012.

Hayo yamebanishwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Neema Rugemayila wakati wa maadhimisho ya siku ya kisukari duniani na kampeni ya mazoezi. 

Amesema silimia 97.2 ya wananchi wanakula mboga mboga na matunda chini ya mara tano kwa wiki  nchini.

Utafiti huo unaonesha kuna ongezeko kubwa la viashiria hivyo linalochangiwa na uvutaji wa sigara na kuwa asilimia 15.9 ya wananchi wanavuta sigara. 

"Asilimia 29.3  wanakunywa  pombe, asilimia 97.2 wanakula mboga mboga na matunda chini ya mara tano kwa wiki, "amesema. 

Amesema asilimia 26 ya wananchi ni wanene kupita kiasi, asilimia 26 wanalehemu nyingi mwilini, asilimia 33.8 wanamafuta mafuta mengi mwilini huku asilimia 9 waligundulika kuwa na kisukari. 

Amesema utafiti huo pia ulionesha asilimia 25 ya wananchi waliohojiwa hawajishughulishi na kazi zinazotumia nguvu na kutofanya mazoezi. 

"Viashiria ambayo tunapaswa kupambana navyo ili tupambane na magonjwa yasiyoambukiza ni unywaji  pombe kupita kiasi, matumizi ya tumbaku na bidhaa zake, ulaji usiofaa hasa matumizi ya chumvi  kwa wingi, mafuta,sukari sukari na kutofanya mazoezi. 

Amesema asilimia 6 ya vifo duniani husababisha na kutofanya mazoezi ambapo imetajwa kuwa ni kiashiria cha nne kinachochangia vifo duniani. 

"Inadaiwa kuwa kutofanya mazoezi kunachagia asilimia  17 ya magonjwa ya moyo na kisukari, asilimia 12 ya matatizo ya kuanguka na asilimia 10 ya saratani ya utumbo maana, "amesema. 

Amesema kwa mujibu wa Shirika la afya duniani(2005), inakadiriwa kuwa asilimia 20 ya vifo vyote vilivyotokea hapa nchini vinatokana na magonjwa yasiyoambukiza. 

Kwa upande wake rais wa Club ya Lion kwa nchi za Tanzania, Uganda na Sudani kusini,  Rowan Qadri amesema wanatoa huduma kwa wagonjwa a kisukari bure kwa wiki moja. 

Amesema kwa pamoja wanaweza kushinda ugonjwa huo hivyo wafunge miili yao ili kupambana a ugonjwa huo. 

Naye Mkurugenzi wa Kinga dhidi ya magonjwa sugu Dk Manase Frank amesema watu wengi wanafariki au kuumia kutokana kutokana na ugonjwa wa kisukari. 

Amewataka viongozi wa dini kuwahubiria waumini kupima afya zao angalau mara moja kwa mwaka. 


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search