TAWA, Polisi wakamata jangili, meno ya tembo.. soma habari kamili na Matukio360.. #share

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Maafisa wa Uhifadhi wa Wanyamapori wamefanikiwa kumkamata jangili akiwa na meno ya Tembo 5 yenye thamani ya MIL 100 name mshitakiwa yuko kituo cha Polisi morogoro.

Sehemu ya shehena ya meno ya tembo iliyokamatwa.
Taarifa kutoka kwa jeshi la Polisi morogoro mshtakiwa anategemea kufikishwa mahakamani. Aidha, Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania - TAWA Bw. Twaha Twaibu ameeleza kuwa walipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwepo kwa jangili huyo wa meno na kutuma maafisa wanyamapori kutoka Makao Makuu ya TAWA wakishirikiana na jeshi la Polisi na kuweza kumkamata jangili huyo.

Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei akiongelea tukio hilo, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliejulikana kwa jina la Nehemiah Nashon akiwa katika chumba namba 104 cha Hoteli ya BZ iliyopo maeneo ya Nane-nane Mjini Morogoro, na kwamba vipande hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi Mil. 100.

Jangili sugu akiwa na shehena ya meno ya tembo akiwa chini ya ulinzi mkali.

Matukio360 imefanikiwa kunasa tukio zima la opersheni na baada ya jangili huyo kudhibitiwa na kuwekwa chini ya ulinzi..



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search