Mbunge ataka wabunge walipwe pensheni...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na
mwandishiwetu
SERIKALI
imeombwa kuanza kuwalipa pensheni wabunge baada ya kuachia wadhifa huo.
Bungeni
Ombi hilo limetolewa leo Bungeni mjini
Dodoma na mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia katika kipindi cha
maswali na majibu.
Katika swali
lake la kwanza
Mbatia aliuliza utaratibu wa kuwahudumia Majaji wastaafu hususani wanapoumwa.
Mbatia amesema sheria ya mwaka 1981 ilielekeza kulipa pensheni wabunge waliondoka katika wadhifa huo na kwamba sasa ni wakati muafaka kwaserikali kuangalia upya utoaji wapensheni kwa wabunge.
“Sheria ya mwaka
1981
kabla yakufutwa ilielekeza wabunge kulipwa pensheni sasa ni muda muafaka kwa serikali kuwapa pensheni wabunge,”
aliuliza Mbatia.
Akijibu hoja hiyo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Antony Mavunde amesema kwakuwa swali ni ombi serikali kabla haijatoa kauli rasmi itaangalia taratibu, sera na sheria ya pensheni ya mwaka 2007 inavyoelekeza.
“Kabla serikali haijatoa tamko rasmi kuhusu ombi hilo, itaangalia taratibu, sera na sheria ya pesheni ya mwaka 2007 inavyoelekeza katika suala hilo,”
alijibu Mavunde
Kuhusu Majaji Wastaafu,
serikali imesema wanahudumiwa kwamujibu wa sheria na taratibu zinavyoelekeza.
No comments:
Post a Comment