Tanzania yaijibu Kenya…Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abraham Ntambara
SERIKALI ya Tanzania imeitaka Serikali
ya Kenya kusubiri majibu sahihi kuhusu ukamatwaji wa vifaranga na mifugo
iliyoingizwa nchini hivi karibuni bila kufuata taratibu na sheria.  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Msimamo huo umetolewa leo jijini Dar
es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.
Augustine Mahiga alipozungumza na waandishi wa habari.
Hatua hiyo inafuatia uchomwaji wa
vifaranga vya kuku wa mayai takribani 6,400 katika eneo la Namanga Mpakani mwa
Tanzania na Kenya ikidaiwa kuingizwa kimagendo. Pia ng’ombe zaidi ya 1,000
walioingizwa kinyemela kwa ajili ya malisho.
“Tanzania inatayarisha maelezo, hata
bungeni  kulikuwa na maswali na tumeandaa
majibu kufafanua tatizo hili,” amesema Dk. Mahiga.
Amesema kwa njisi tatizo hilo linavyoripotiwa
linaleta sintofahamu kwa nchi zote mbili.
Dk. Mahiga amesema zipo  sheria na taratibu za mifugo ambazo hazimo
kwenye makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Amesema  majibu ya suala hilo yatatolewa na wizara yake
na wizara ya  mifugo na uvuvi.




No comments:
Post a Comment