MOI kujenga maabara ya kisasa...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Salha Mohamed
TAASISI
ya Tiba ya Mifupa(MOI), imesema maabara
ya kisasa itakayopima vipimo vyote vya damu itaanzishwa mara baada ya
kukamilika kwa mradi wa jengo la MOI awamu ya tatu.
Meneja Uhusiano Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Jumaa Almasi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mafanikio ya taasisi hiyo na kumpongeza rais John Magufuli katika kipindi cha miaka miwili leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni ofisa Uhusiano wa taasisi hiyo Patrick Mvungi.
Pia
imesema serikali imetoa bilioni 16.5 kununua vifaa tiba vya uchunguzi ikiwamo
CT-Scan, MRI, X-ray 2, C-arm na ultrasound ya kisasa.
Hayo
yamesemwa Dar es Salaam na Meneja
uhusiano wa Taasisi hiyo, Jumaa Almas wakati akizungumza na waandishi wa habari
alipokuwa akizungumzia mafanikio yaliyopatikna katika kipindi cha miaka miwili(
2015/2017) na jitihada za rais Magufuli
katika sekta ya afya.
Amesema
kukamilika kwa jengo hilo kutaanzishwa kwa maabara ya kisasa ambayo itafanya
vipimo vyote vya damu, kuongeza vitanda vya ICU kutoka vitanda 8 hadi 32.
"Kutaanzishwa
kwa kitengo kipya cha kisasa cha wagonjwa ya dharura na tutaongeza vyumba viwili vya upasuaji na kufanya taasisi
kuwa na vitanda 8,"amesema.
Amesema
katika kipindi cha miaka miwili taasisi hiyo
imetengeneza viungo bandia 1362 kutokana
na serikali kurahisisha upatikanaji w malighafi za kutengeneza hapa nchini
ambapo awali wengi walihitaji kupelekwa nje ya nchi kwa gharama kubwa.
Amesema
wamekuwa na ongezeko la wagonjwa wanaopewa huduma za kibingwa (Super
Specialised services) ambapo wamefanya upasuaji mkubwa kwa wagonjwa 221 wa
nyonga(Total hip replacement.
Almas
ameongeza wamefanya upasuaji wa mgongo kwa wagonjwa 259(Specialized spine
survey), 306 wagonjwa wa
ubongo(Specialized brain surgery), upasuaji wa matundu (Athroscopy) kwa wagonjwa 314, watoto wenye vichwa vikubwa
a mgongo wazi (Hydrocephalus and Spina bifida)
852, wagonjwa 120 wa upasuaji wa magoti (Total Knee replacement),
Upasuaji wa mfupa wa kiuno (Acetabular reconstruction) kwa wagonjwa 114.
"Upasuaji
mwingine wa mifupa tumefanya kwa wagonjwa 8615.Idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa
upasuaji imeongeza kutoka wagonjwa 300-400kwa mwezi hadi kufikia wagonjwa 600-700 kwa
mwezi,"amesema.
Almas
amesema "Hili limewezekana kutokana na serikali kuongeza upatikanaji wa
vifaa tiba na nafasi ya kulaza wagonjwa ambapo awali ilikuwa finyu,"
amesema.
Amesema
awali mazingira ya kutokea huduma yalikuwa hatarishi kwa watumishi na wagonjwa
kupata maambukizi kutokana na ufinyu wa nafasi na idadi kubwa ya wagonjwa.
Amesema
kuanza kukamilika kwa mradi wa awamu ya tatu kumesababisha mazingira ya kazi
kuwa rafiki kwa watoa huduma n wagonjwa pia.
"Idadi
ya wagonjwa ilikuwa kubwa kwa mfano wodi ya yenye vitanda 33 ilikuwa inalaza
wagonjwa 90 hadi 100,"amesema Almas.
Amesema
katika kipindi cha miaka miwili taasisi hiyo imeongeza idadi ya vitanda kutoka
159 hadi kufikia vitanda 340 baada a rais Magufuli kutoa maelekezo ya wagonjwa
kutopata huduma wakiwa wamelazwa chini.
"Kimsingi
suala la wagonjwa kulala chini MOI limebaki historia, mazingira ya kutoa huduma
yameboreshwa, "amesema.
No comments:
Post a Comment