Maalbino kutibiwa bure...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
SERIKALI ipo katika mkakati
wa kuandaa utaratibu na sera ya matibabu
bure kwa watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali Bungeni
Pia itawadhibiti
wafanyabiashara wanaouza mafuta ya ngozi ya Albino kwa bei ya juu.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni
mjini Dodoma na naibu waziri ofisi ya waziri mkuu, Stella Alex Ikupa alipokuwa
akijibu swali la mbunge juu ya mpango wa serikali kuondoa kodi ya dawa na mafuta
ya ngozi yanayotumiwa na Albino.
"Pamoja na mambo mengine Serikali
inaanda utaratibu na sera ya matibabu bure kwa watu wenye ulemavu wa
ngozi(Albino). Pia itawadhibiti wote wanaouza dawa na mafuta ya ngozi ya Albino
kwa bei ya juu," amesema Ikupa
Amesema serikali imeshaondoa
kodi ya dawa zote za watu wenye ulemavu ikiwamo mafuta ya ngozi ya albino.
Kuhusu upungufu wa dawa naibu
waziri huyo amesema serikali itaendelea kuagiza dawa za Albino kadri itakavyohitajika.
"Serikali itaendelea kuagiza dawa za watu wenye ulemavu wa ngozi kadri zitakavyohitajika," amesema
No comments:
Post a Comment