Msemaji wa Serikali: Nchi imetikisika!...soma habari kamili na Matukio360..#share

Na mwandishi wetu
MSEMAJI mkuu wa
serikali na mkurugenzi mkuu wa idara ya habari maelezo, Dk Hassan Abass amesema
kwa sasa nchi imepata mshtuko.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dk Hassan Abass
Amesema hayo leo jijini
Dar es salaam alipokuwa akitoa tathmini ya miaka miwili ya serikali ya awamu ya
tano tangu iingie madarakani Novemba 5, 2015.
“Pamoja na mambo mengine changamoto katika
miaka hii miwili ya uongozi wa rais Dk Magufuli ni mshtuko wa ndani na nje ya nchi ya jinsi Tanzania
inavyofanya shughuli zake, nchi imetikisika,” amesema Abbas
Amesema imetigisika
kufuatia wapiga dili kushindwa kufanikisha
mipango yao ya kujipatia kipato kwa njia ya ‘ujanja’ kutokana na mianya yote
kubanwa na kudhibitiwa ipasavyo na serikali.
Dk Abass amesema kutokana
na hali hiyo wapo watu wa ndani na nje ya nchi wasiofurahia jitihada hizo na
amewataka watanzania kushikamana katika
hilo na kudhibiti maslahi ya taifa.
“Wengi wa wapiga dili
ambao walizoea kujipatia fedha ndivyo sivyo wameshikwaa na butwaa na
hawafurahia hali hii, ukweli mianya imebanwa ipasavyo hivyo si wa ndani wala wa
nje hawafurahii hali hii,” amesema Abass.
Kuhusu mafanikio
katika sekta mbalimbali amesema serikali
imefanya jitihada za kutosha na kwamba mafanikio yanaanza kuonekana.
Katika sekta ya elimu
amesema kila mwezi serikali inatoa bilioni 23
kugharamia elimu bure, sekta ya afya dawa zinapatikana na uanzishwaji wa viwanda
vitakavyosaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.
Msemaji huyo wa
serikali amesema hadi kufikia mwisho wa Novemba, 2017 serikali itapandisha
madaraja wafanyakazi na kuongeza mishahara.
“Pia serikali inatoa
ajira 52000 katika sekta mbalimbali hii ni kabla ya mwisho wa bajeti tayari
zingine zimeanza kutangazwa ikiwamo maafisa kodi wa TRA, maafisa wa afya. Na
imewafukuza watumishi takribni 1200 wa
vyeti feki na elfu ishirini hewa,” amesema
Kuhusu ndege, amesema
hadi kufikia Julai, 2018 ndege zote zilizonunuliwa na serikali zitafika nchini.
“Ndege ya Boing
itaingi Julai na cc series zitaingia June,
2017 nyingine zipo katika majaribio na hadi mwakani mwanzoni zitakuwa zimefika nchini,” amesema
No comments:
Post a Comment