ACT wampa neno rais Magufuli...soma habari kamili na matukio360..#share

Abraham Ntambara

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimemtaka rais Dk John Magufuli kuacha kuongoza nchi kibaguzi  ili  akumbukwe kwa historia njema atakapomaliza  uongozi wake
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Yeremia Maganja (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ( pichami hawapo)

Pia kimesema mwenyekiti na katibu mkuu wa chama hicho wataitikia wito wa Jeshi la Polisi kwenda kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kitengo cha Makosa ya Fedha (Financial Crime)  na si  kamati kuu ya chama hicho.

Msimamo huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na kaimu mwenyekiti wa chama hicho, Yeremia Maganja  alipozungumza na waandishi wa habari na kwamba rais Magufuli na CCM wanasera  ya kubagua watu kwa misingi ya kisiasa.

“Magufuli amesahau kwamba alipata asilimia 58 za kura, upinzani ulipata asilimia 42, kwa hiyo katika kila watanzania 10 kuna watanzania 4 wa vyama mbadala, hawa ni Watanzania ambao kijamii wanabaguliwa,” amesema Maganja.

Amesema  kwa sasa watu wanaotoa maoni au mawazo mbadala na serikali wanachukiwa na kukumbwa na misukosuko ikiwemo kukamatwa na jeshi la polisi.

Maganja amesema taifa lisilohoji ni taifa la wajinga na  ametaka kuwapo kwa uhuru wa maoni kwa kila mtanzania.

Kuhusu wito wa kuitwa na jeshi la polis, Maganja amesema Novemba 2, 2017 walipokea wito  huo ukiwataka  wajumbe wa kamati kuu ya ACT-Wazalendo kufika kituo cha pilisi cha Kamata, Kariakoo jijini Dar es Salaam kwenda kuhojiwa na DCI.

Amesema wito huo ni  kufuatia taarifa ya ACT Wazalendo  waliyoitoa kuhusu kusinyaa kwa uchumi na kuwa serikali inapika takwimu za uchumi nchini

"Kamati kuu ni chombo cha kitaifa chenye mamlaka ya kufanya maamuzi kwa mujibu wa katiba ya ACT kama chombo na si kama mjumbe mmoja mmoja. Jeshi la Polisi halina madaraka ya kushughulikia wa kuingilia maamuzi  halali ya vyombo (organs) katika vyama vya siasa," amesema

Naye katibu wa itikadi, uenezi na mawasiliano wa chama hicho  Ado Shaibu amesema  kamati kuu ni  katibu mkuu, wenyeviti wote wa bara na visiwani, manaibu makatibu wakuu, wenyeviti na wajumbe.

"Hivyo vigumu kwa kamati yote kuripoti kutokana na wajumbe  wanatoka sehemu mbalimbali nchini lakini pia anayeweza kuwa sahihi kutoa taarifa za kikao ni katibu mkuu au mwenyekiti wa chama," amesema

Pamoja na mambo mengine amesema kazi ya Jeshi la Polisi si masuala ya kisiasa ni kulinda usalama wa raia.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search