Mugabe, mkewe ‘bye bye’ Zanu-PF yawatosa...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
CHAMA tawala nchini Zimbabwe
Zanu-PF kimemfuta Robert Mugabe kama kiongozi wake na Grace Mugabe ambaye
alikuwa mwenyekiti wa taifa wa wanawake.
Pia kimemfuta waziri wa elimu Jonathan Moyo na waziri wa serikali za mitaa, Saviour Kasukuwere
Pia kimemfuta waziri wa elimu Jonathan Moyo na waziri wa serikali za mitaa, Saviour Kasukuwere
Mr Robert Mugabe akiwa na mke Grace Mugabe wakiwa wamevalia mavazi ya chama cha Zanu-PF
Kimemtua aliyekuwa makamu wa
rais, Emmerson Mnangagwa ambaye alifutwa wiki mbili zilizopita kama kiongozi
wake.
Mkuu wa chama chenye nguvu
cha wale waliopigania uhuru Chris Mutsvangwa, aliiambia Reuters kuwa chama
kilikuwa kinaanza mchakato wa kumuondoa Mugabe madarakani kama rais.
Zanu-PF ndio chama
kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40. Lakini sasa inabidi
wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala.
Hata hivyo kufutwa kwa Mnangawa kumezua mambo mengi huku jeshi
likitwaa madaraka na kumzuia Mugabe mwenye umri wa miaka 93, kumteua mke wake,
Grace kama makam wa rais.
Jana waandamanaji walipiga
kambi nje ya makao ya Mugabe kumshinikiza kujiuzulu. Maelfu ya watu nchini
Zimbabwe waliingia barabarani siku ya Ijumaa kuandamana kumpinga Mugabe.
Mugabe anatarajiwa kukutana
na makanda wa jeshi na msafara wa magari umeonekana ukiondoka makao ya rais.
Jeshi la nchi hiyo
lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani
tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina.
Mugabe angependelea mkewe
kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa
Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na
uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa
madaraka.
No comments:
Post a Comment